Haji Manara Akomaa Na Yanga, Amumwagia Sifa Okwi.Soma Zaidi Hapa...


Afisa habari wa klabu ya Simba sports,Haji Manara amemumwagia sifa Mshambuliaji wa klabu hiyo Emmanuel Okwi kutokana na Kiwango ambacho nyota huyo amekionyesha katika michezo yake miwili ya Ligi kuu msimu huu.

Okwi ambae ameng'ara kwa kuzifumania nyavu za wapinzani wa Simba mara 6 katika michezo miwili pekee amekua kivutio kwa msemaji huyo huku msemaji huyo akirusha makombora kwa wale wote waliokua wakimuita Okwi,Mhenga.

Manara kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika"Mpira wakati mwingine hautendi haki,Gongowazi game tatu wamepata goli tatu,waliomwita Mhenga,Okwinho kacheza game moja goli nne!!aibu yao au yetu?" Kauli hii aliitoa saa chache kabla ya Mchezo kati ya Simba na Mwadui.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika Manara akaandika hivi,"East Africa ina Okwi mmoja tu,,Game mbili goli sita,mara mbili ya magoli yote ya Gongowazi kwa game zao tatu!!kosa lao lilikuwa kumwita mhenga,,atashinda kila tuzo nchi hii,THIS IS Simba and THAT is Okwinho"

Hata hivyo Mashambulio hayo ya Manara yanawalenga wapinzani wa jadi wa Simba ambao nia Yanga Sc.

Ili kupata updates kamili kuhusu habari hii na nyinginezo nyingi Download app yetu HAPA bure kufurahia habari kali za michezo kila siku,pia usisite kututumia maoni yako. USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPO CHINI,PIA TUACHIE MAONI YAKO.
NA KWA HABARI YOYOTE YA MICHEZO USISITE KUTUTUMIA KWENYE WHATSAPP NO:0656800588

No comments: