Yusuph Manji na wengine watatu, wasomewa Mashtaka ya kuhujumu Uchumi. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 5 July 2017

Yusuph Manji na wengine watatu, wasomewa Mashtaka ya kuhujumu Uchumi.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemsomea Mashtaka saba Mwenyekiti wa Quality Group na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Manji na wenzake watatu yakiwamo ya Uhujumu uchumi na usalama wa nchi.
Kesi ambayo walisomewa Kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alipolazwa Mtuhumiwa namba moja Yusuph Manji, Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Kisutu Huruma Shahidi na Wakili wa Serikali Kishenyi Mitalemwa. 
Watuhumiwa wengine ni Pamoja na Abdala Sangey,  Deogratias Kisimba, na Tobias Fwele. Shitaka la Kwanza. 
Inadaiwa kuwa Juni 30, 2017 eneo la Changombe  Temeke Jijini Dar es Salaam washakuwa walikutwa na Askari Polisi wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa yanayotumika kutengenezea Sare  za Polisi zenye Thamani ya Milioni 192.5.
Shtaka la Pili watuhumiwa wote Tarehe 30 Juni walikutwa na Mabando Manane ya vitambaa zinazotumika kutengeneza Sare za jeshi la Wanachi 'JWTZ'. 
Kosa la Tatu watuhumiwa walikukutwa na mihuri ya serikali Ambapo washtakiwa wote  kwa pamoja tarehe 1 Julai walikutwa na mihuri ya jeshi la Tanzania iliyoandikwa  "Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha jeshi JWTZ " bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatarisha usalama wa nchi. 
Kosa Nne watuhumiwa walikutwa na Mhuri wa JWTZ  yenye maandishi  Kamanda kikosi 834 KJ Makutupola Dodoma bila kuwa na uhalali WA kitendo hicho. 
Shtaka la tano ni kukutwa na Mhuri wa Serikali wenye maneno "COMMANDING Oficer 835 kj Mgambo P.O.BOX...".
Kosa la Sita. 
Shtaka la sita ni kukutwa na mali inayozaniwa kupatikana isivyo halali Tarehe 1 Julai eneo la Changombe Plot namba SU 383 ambayo ilipatakana isivyo halali. washtakiwa Hawakuruhusiwa kujibu mashtaka hayo kwa sababu wanashtakiwa kwa sheria ya Uhujumu Uchumi na usalama wa Taifa. 
Hakimu Shahidi amesma  Kwamba masuala hayo yasikilizwe kwenye Mahakama yenye mamlaka. 
Kesi hiyo itatajwa tena Tarehe 19 mwezi Julai Huku bado upelelezi wa Kesi hiyo ukitajwa kuwa haujakamilika.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages