Usajili: Everton yazidi kuvunja kibubu.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 4 July 2017

Usajili: Everton yazidi kuvunja kibubu..

Usipitwe na habari zetu kwa download application yetu ambayo kwa sasa ipo playstore kwa jina la VYANKENDE BLOG au bofya HAPA kudownload na uweze kusoma habari zetu bila ya kua na MBKlabu ya Everton imeendelea kumwaga fedha kusajili kujijenga kwa msimu ujao, baada ya leo kukamilisha uhamisho wa beki wa kati wa zamani wa Manchester United, Michael Keane kutoka Burnley kwa ada ya uhamisho ya rekodi, Pauni Milioni 30.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano kuhamishia kazi zake Uwanja wa Goodison Park.

Na Keane anakuwa mcheaji wa tano kusajiliwa na kikosi cha kocha Ronald Koeman katika dirisha hili la usajili, kuashiria timu hiyo inayodhaminiwa na SportPesa imedhamiria 'kujiumba upya'.

Keane anasajiliwa Everton baada ya timu hiyo ambayo wiki ijayo itakuja Tanzania kucheza na Gor Mahia ya Kenya kuwsajli pia kipa Jordan Pickford, kiungo Davy Klaasen na washambuliaji Sandro Ramirez na Henry Onyekuru ambao kwa pamoja wanafanya klabu hiyo itumie jumla ya Pauni milioni 96 kusajili.

Manchester United inatarajiwa kupata hadi Pauni Milioni 7.5 katika dili hilo, ikiwa ni asilimia 25 ya mauzo baada ya makubaliano wakati Keane anaondoka Old Trafford kwenda Burnley mwaka 2015.
Kocha wa Toffees, Koeman anaamini Keane ataendelea kuimarika.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages