Tisa kamati ya utendaji TFF waupotezea uchaguzi. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 8 July 2017

Tisa kamati ya utendaji TFF waupotezea uchaguzi.


WAJUMBE tisa wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) inayomaliza muda wake, wameupotezea uchaguzi wa shirikisho hilo utakaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma.
Wakati wenzao 13 wakiamua kujitosa kwenye uchaguzi huo kusaka nafasi ya kurudi TFF kwa kuchaguliwa ili kuziwakilisha kanda mbalimbali kisoka, wajumbe hao tisa wameonekana kukwepa vita ya kuwania uwakilishi katika chombo hicho chenye mamlaka ya kusimamia soka nchini.
Sura tisa za kamati hiyo zilizojiweka kando katika uchaguzi wa awamu hii ni Ahmed Mgoyi, Wilfred Kidau, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, Yahya Mohammed, Richard Sinamtwa, Epafra Swai, Paul Marialle, Blassy Kiondo na Mwesigwa Celestine.
Nafasi pekee kwa wajumbe hao tisa kurudi kwenye Kamati ya Utendaji ya TFF, ni kupitia uteuzi wa Rais atakayechaguliwa ambaye Katiba ya shirikisho hilo inampa fursa ya kuteua wajumbe wawili wa kamati hiyo.Kati ya wajumbe hao tisa, wawili ambao ni Kidau na Mgoyi walitangaza hadharani uamuzi wa kutotetea nafasi zao wakati waliosalia hawakusema kitu na hawamo kwenye mchakato.
Hata hivyo wakati wajumbe hao tisa wakiamua kutoingia vitani kuwania nafasi, wajumbe 13 wapo kwenye mchakato wa uchaguzi wakiwania nafasi mbalimbali.
Wajumbe hao na nafasi wanazogombea ni; Jamal Malinzi na Wallace Karia (Urais) wakati ujumbe wa kamati ya utendaji ni Salum Chama, Kaliro Samson, Omary Walii, Vedastus Lufano, James Mhagama, Athuman Kambi, Hussein Mwamba, Ayoub Nyenzi, Khalid Mohammed, Ramadhan Nassib na Rose Kisiwa.
Uchaguzi huo umezua gumzo kubwa na unaonekana kujaa upinzani baada ya kusababisha kamati ya uchaguzi kuvunjwa na kuundwa mpya.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages