Tetesi za Usajili Ulaya leo July 14. 2017. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 14 July 2017

Tetesi za Usajili Ulaya leo July 14. 2017.

Ungana nasi kila siku kwa habari mbalimbali za michezo kitaifa na kimataifa ,tetesi mbalimbali za Usajili bila kusahau magazeti kila siku kwa kudownload application yetu leo.BOFYA HAPA KKUDOWNLDKocha Pep Guardiola amejitosa katika foleni ya makocha na vilabu vinavyojaribu kumshawishi kinda aliye matawi ya juu, Kylian Mbappe kujiunga na Manchester City.
Baada ya tetesi kutawala kuwa atatimkia Barcelona, beki wa Arsenal, Hector Bellerin ameonesha ishara ya kuendelea kubaki Emirates kwa kuweka picha akipiga mbizi na kuahidi kumfundisha mchezaji mwenzake Mustafi atakaporejea.
Ofa ya Liverpool ya pauni milioni 57 kumnunua kiungo Naby Keita imekataliwa na klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani.
Chelsea na Liverpool zimeingia katika vita kubwa ya kumwamina mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang mwenye thamani ya pauni milioni 65.
Arsenal inajiandaa kumuuza kwa jumla kiungo wake Jack Wilshere kwa klabu ya Sampdoria kwa dau la pauni milioni 9.
Kocha Jose Mourinho yuko mbioni kutenga dau la kumrudisha kundini mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic baada ya kuelekea kupona  apema kinyume na matarajio ya awali kuwa angekaa nje zaidi ya mwaka.

Chelsea watakamilisha usajili wa kiungo Tiemoue Bakayoko, 22, kutoka Monaco kwa pauni milioni 39.7 katika saa 24 zijazo, ingawa mchezaji huyo atakosa mechi kadhaa za mwanzo kutokana na kuwa majeruhi. (Daily Express)

Kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27, atakataa kwenda Leicester kwa sababu anataka kujiunga na Everton. (Leicester Mercury)

Liverpool na Chelsea wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, ambaye thamani yake ni pauni milioni 65. (Sun)
Kipa wa Manchester United David de Gea, 26, anataka kujiunga na Real Madrid msimu huu na amemuambia wakala wake Jorge Mendes kufanikisha uhamisho wake. (Don Balon)

Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22. (Daily Mirror)

West Ham wanakaribia kukamilisha usajili wa mkopo wa kipa wa Manchester City Joe Hart, 30. (Independent)

Newcastle watapewa nafasi ya kumsajili kipa wa West Ham Darren Randolp, ikiwa Joe Hart atakwenda West Ham. (Newcastle Chronicle)

Roma wametoa dau la pauni milioni 29 kumtaka Riyad Mahrez, 26, lakini Leicester wanataka pauni milioni 50. (London Evening Standard)


Ungana nasi kila siku kwa habari mbalimbali za michezo kitaifa na kimataifa ,tetesi mbalimbali za Usajili bila kusahau magazeti kila siku kwa kudownload application yetu leo.BOFYA HAPA KKUDOWNLD


Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka uhamisho wa Kyle Walker, 27, kwenda Man City uharakishwe ili wapate fedha za kusajili wachezaji wengine. (Daily Mail)

Tottenham wanatarajia kuziba pengo la Kyle Walker kwa kumsajili beki wa Porto Rocardo Pereira, 23, kwa pauni milioni 22. (Times)

Tottenham wanakaribia kukamilisha usajili wa beki Juan Foyth, 19, kutoka Estudiantes, ambaye atakuwa usajili wa kwanza wa Spurs msimu huu. (ESPN)


Ungana nasi kila siku kwa habari mbalimbali za michezo kitaifa na kimataifa ,tetesi mbalimbali za Usajili bila kusahau magazeti kila siku kwa kudownload application yetu leo.BOFYA HAPA KKUDOWNLD


No comments:

Post Bottom Ad

Pages