Tetesi za Usajili Ulaya leo July. 07. 2017 - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 7 July 2017

Tetesi za Usajili Ulaya leo July. 07. 2017MUSTAKABALI WA CONTE CHELSEA U HATIANI

Chelsea kushindwa kusajili wachezaji waliokuwa wakiwataka majira ya joto kumeiweka shakani nafasi ya Conte katika klabu hiyo, kwa mujibu wa Mirror .

Romelu Lukaku akiwa anakaribia kujiunga na Manchester United, klabu imeshindwa kumpata Alexis Sanchez na Virgil van Dijk huku wakiwa wanahaha kumsajili Alex Sandro na Tiemoue Bakayoko, Muitaliano huyo amezidi kupandwa na jazba.

Imeripotiwa kuwa meneja huyo amewakasirikia viongozi wa klabu hiyo kushindwa kumsajili Lukaku anayekaribia kutua Man United. 

MILAN YAMGEUKIA AUBAMEYANG

Milan wanamgeukia Pierre-Emerick Aubameyang kuimarisha safu yao ya mashambulizi, kadhalika klabu hiyo inataka kumsajili Nikola Kalinic, kwa mujibu wa  Gianluca Di Marzio .

Klabu hiyo ya Italia inataka kulipa ada wanayotaka Borussia Dormtund na kukamilisha mazungumzo na mchezaji huyo. 

BARCA YAMRUDIA PAULINHO

Licha ya ofa kwa ajili ya Paulinho kukataliwa na Guangzhou Evergrande ya China, Barcelona wapo tayari kutoa ofa nyingine, limeripoti Cadena SER .

Klabu hiyo ipo tayari kuimarisha ofa yao ya euro milioni 20 kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 baada ya wachezaji wengine waliokuwa wakiwahitaji kuwa ngumu kuwapata. 

ALEXIS ANATAKA £400,000 KWA WIKI

Alexis Sanchez anadai ujira wa £400,000 ili kusaini mkataba mpya na klabu ya Arsenal, kwa mujibu wa Mirror .

Miamba hao wa Emirates wamempa kiasi cha paundi 275,000 tayari, lakini mchezaji huyo anaonekana kutoridhika na Arsenal hawapo tayari kumwongezea nachotaka ingawa hawana mpango wa kumuuza kwa Manchester City. 

MBAPPE APIGIWA TENA SIMU NA MADRID

Real Madrid imempigia upya simu Kylian Mbappe, klabu hiyo haijakata tamaa kumfukuzia mchezaji huyo kinda wa Monaco, kwa mujibu wa Marca .  

MARSEILLE INAAMINI ITAMPATA GIROUD

Marseille wanajiamini wataweza kumrejesha Olivier Giroud Ligue 1 kutoka Arsenal, kwa mujibu wa Telegraph .

PSG WATENGA €80M KWA AJILI YA COUTINHO

PSG wamepania kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho ikiwa watashindwa kumsajili Kylian Mbappe kutoka Monaco, kwa Le10sport .

Mbappe anaweza kubaki Monaco, hivyo PSG italazimika kuangalia kwingine kupata mchezaji wanayemtaka kuimarisha safu yao ya mashambulizi. Klabu hiyo ya Ligue 1 imeandaa kitita cha euro milioni 80 kumsajili Mbrazili Coutinho, lakini Liverpool wanataka euro milioni 100.

LEICESTER YAKARIBIA KUMSAJILI IHEANACHO

Leicester City wameipiku West Ham kuinasa saini ya mshambuliaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, kwa mujibu wa ESPNFC .

BARCA IPO TAYARI KUMSAJILI BELLERIN

Barcelona wapo tayari kutoa paundi milioni 26 kwa ajili ya kiungo wa Arsenal Hector Bellerin, kimedai chanzo cha Hispania Sport .

Miamba hao wa La Liga wanataka kumrejesha Catalan beki huyo ambaye wamemkuza wenyewe kwenye akademi yao.

ARSENAL YAMFUKUZIA FABINHO

Arsenal wanafuatilia kwa karibu maendeleo yote yanayohusu mustakabali wa kiungo wa Monaco, Fabinho, kwa mujibu wa France Football .

Manchester United pia wamekuwa karibu sana wakimfuatilia mchezaji huyo lakini hawakufikia popote.

CHELSEA YATENGA DAU KWA AJILI YA JAMES

Chelsea wameandaa mezani dau nono kwa ajili ya kiungo wa Real Madrid James Rodriguez, limeripoti AS .

Mkolombia huyo anatarajiwa kuondoka Bernabeu majira ya joto, Manchester United na PSG zikiwa zinamtamani pia.

BALE ANAWEZA KUONDOKA KWA PAUNDI MIL 88

Real Madrid watakuwa tayari kumuuza Gareth Bale iwapo paundi milioni 88 zitatolewa kwa ajili yake, kimeripoti Diario Gol .

Manchester United ni miongoni mwa klabu zinazoitamani huduma ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales.

ATLETI KUMPELEKA COSTA CHINA KWA MKOPO

Mipango ya Atletico Madrid kuinasa saini ya Diego Costa inaweza kumpeleka China kwa mkopo hadi watakapoweza kumsajili, limeripoti Mirror .

Klabu hiyo ya La Liga ipo tayari kuzungumza na mshambuliaji huyo wa Chelsea, lakini uwezo wao wa kifedha kumsajili unawaruhusu tu kumpeleka kwa mkopo hadi adhabu yao ya kufungiwa itakapoisha Januari.

CHELSEA YAKUBALI KUMSAJILI RUDIGER

Chelsea imefikia makubaliano kumsajili beki wa Roma na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Antonio Rudiger, kwa mujibu wa Sports.

LIVERPOOL YAAMUA KUMPOTEZEA KEITA

Liverpool imeacha kumfukuzia Keita Balde wa Lazio baada ya ofa yao ya paundi milioni 30 kukataliwa, kimedai Calciomercato.com .

ARSENAL KUTOA OFA MPYA KUMSAJILI LEMAR

Arsenal wanataka kutoa ofa iliyochangamka kumpata winga wa Monaco Thomas Lemar baada ya kumsajili mshambuliaji Alexandre Lacazette, kwa mujibu wa Evening Standard .

No comments:

Post Bottom Ad

Pages