Tetesi za Usajili Ulaya leo July. 06. 2017. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 6 July 2017

Tetesi za Usajili Ulaya leo July. 06. 2017.ATLETI KUMPELEKA COSTA CHINA KWA MKOPO


Diego Costa Chelsea Premier League

Mipango ya Atletico Madrid kuinasa saini ya Diego Costa inaweza kumpeleka China kwa mkopo hadi watakapoweza kumsajili, limeripoti Mirror .
Klabu hiyo ya La Liga ipo tayari kuzungumza na mshambuliaji huyo wa Chelsea, lakini uwezo wao wa kifedha kumsajili unawaruhusu tu kumpeleka kwa mkopo hadi adhabu yao ya kufungiwa itakapoisha Januari.

CHELSEA YAKUBALI KUMSAJILI RUDIGER


Antonio Rudiger Germany press conference 17062017
Chelsea imefikia makubaliano kumsajili beki wa Roma na mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Antonio Rudiger, kwa mujibu wa Sports.

LIVERPOOL YAAMUA KUMPOTEZEA KEITA


Balde Keita Lazio
Liverpool imeacha kumfukuzia Keita Balde wa Lazio baada ya ofa yao ya paundi milioni 30 kukataliwa, kimedai Calciomercato.com .

ARSENAL KUTOA OFA MPYA KUMSAJILI LEMAR


HD Thomas Lemar Monaco
Arsenal wanataka kutoa ofa iliyochangamka kumpata winga wa Monaco Thomas Lemar baada ya kumsajili mshambuliaji Alexandre Lacazette, kwa mujibu wa Evening Standard .

LYON WASAKA MRITHI WA LACAZETTE


HD Munir El Haddadi Barcelona
Lyon wanajipanga kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Munir El Haddadi kuchukua nafasi ya Alexandre Lacazette aliyetimkia Arsenal, limeripoti Sport .

PSG YAJIPANGA UPYA KUMSAJILI MBAPPE


Kylian Mbappe Monaco
Paris Saint-Germain wanamuandalia dau jipya nyota wa Monaco Kylian Mbappe na wameshawasiliana na wawakilishi wa mchezaji huyo kwa mujibu wa L'Equipe.

ARSENAL KUKUTANA NA ALEXIS WIKI HII


Alexis Sanchez Arsenal
Arsene Wenger atakutana na Alexis Sanchez na Hector Bellerin wiki hii kuwashawishi kubaki Arsenal msimu ujao, limeripoti gazeti la The Sun.
Alexis anataka kujiunga na Manchester City wiki chache zijazo, licha ya Wenger kutamka wazi wazi kuwa Gunners hawana mpango wa kumuuza kwa wapinzani wao wa Ligi Kuu.
Bellerin amekuwa kwenye rada za Barcelona kwa muda mrefu, ingawa bosi wa Arsenal ameshasema Mhispania huyo hataruhusiwa kuondoka.

DONNARUMMA AKUBALI DILI LA MILAN


Gianluigi Donnarumma Italy U21
Gianluigi Donnarumma amekataa kujiunga na Paris Saint-Germain na amekubali kusiani mkataba mpya AC Milan, kwa mujibu wa Sky Sport Italia.

COSTA AKATAA KWENDA CHINA


Diego Costa HD
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amekataa kujiunga na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya China, kwa mujibu wa habari kutoka Daily Mirror.

MOURINHO HANA FURAHA MAN UTD


Jose Mourinho Manchester United
Jose Mourinho hana furaha Manchester United baada ya klabu hiyo kushindwa kuwasajili wachezaji aliopendekeza waletwe Old Trafford, limeripoti Guardian
Usajili wa Nemanja Matic, Alvaro Morata na Ivan Perisic unadorora, Mourinho amekerwa na uzito wa klabu hiyo kufanya usajili kwani hatakuwa na kikosi kamili katika maandalizi ya msimu mpya.

LIVERPOOL YAANDAA DILI LA RICO


Sergio Rico Sevilla Atletico Madrid La Liga 23102016
Liverpool wanaandaa dau la euro milioni 12 kwa ajili ya kipa wa Sevilla, Sergio Rico kwa mujibu wa ABC de Sevilla.

WEST HAM YAMGEUKIA CHICHARITO


Javier Chicharito Hernandez Mexico
West Ham wamemfanya mshambulizi wa Bayer Leverkusen Javier Hernandez 'Chicharito' mshambuliaji chaguo la kwanza katika usajili wa majira ya joto.

CONTE AMTAKA LUKAKU HATA KWA £100M


Romelu Lukaku
Antonio Conte ameitaka Chelsea kutumia paundi milioni 100 kumsajili Romelu Lukaku, ikiwa jambo hilo litafanikiwa, mshambuliaji huyo wa Everton atatua Darajani majira ya joto, kwa mujibu wa The Telegraph .
Conte anaamini Lukaku atakuwa mbadala sahihi kwa Diego Costa aliyeko kwenye rada za Atletico Madrid, lakini pia Manchester United wanataka kumsajili Lukaku.

BARCA YAONGOZA MBIO KUMWANIA BONUCCI


Leonardo Bonucci Juventus
Barcelona wanaongoza katika mbio za kumwania beki wa Juventus Leonardo Bonucci, kwa mujibu wa Daily Mirror .
Chelsea walikuwa na tumaini la kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Italia, lakini beki huyo wa kati anapendelea kujiunga na Barcelona iwapo ataondoka Juventus.

SWANSEA YAMTAKA CHALOBAH KWA MKOPO


Nathaniel Chalobah
Swansea City wanataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa Chelsea Nathaniel Chaloba, kwa mujibu wa  Daily Mirror .

KEITA AANZA MAZUNGUMZO YA MUSTAKABALI WAKE


HD Naby Keita
Jurgen Klopp ameitaka Liverpool kuanza kuchukua hatua kumsajili Naby Keita mchezaji huyo anapojiandaa kuzungumzia mustakabali wake na RB Leipzig, kimeripoti  The Times .
Keita ni shabaha ya kwanza kwa Klopp anayetaka kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kampeni za msimu mpya wa Ligi Kuu Uingereza na Ligi ya Mabingwa Ulaya Uefa.
Leipzig hawataki kumuuza Keita wakiwa wameitaja thamani yake kuwa euro milioni 80 huku Liverpool wakiwa wamemtengea ujira wa paundi 130,000 kwa wiki.

LIVERPOOL WAITAJA THAMANI YA COUTINHO KUWA €100M


Philippe Coutinho Liverpool Premier League
Liverpool wameiambia Paris Saint-Germain kuwa Philippe Coutinho atagharimu €100 millioni baada ya kumuulizia Mbrazili huyo, The Mirror limeripoti.
PSG wameungana na Barcelona kuonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo, lakini Liverpool hawana mpango wa kumuuza dirisha la uhamisho wa majira ya joto na wamejaribu kuzifukuza mbali timu zinazomtaka kwa kutaja dau kubwa mno.

CHELSEA YAMUWINDA DANILO


Danilo Real Madrid
Chelsea imeungana na Juventus kumfukuzia Danilo, Real Madrid ikiwa imejiandaa kumuuza beki huyo wa kulia ikiwa watapokea ofa isiyopungua euro milioni 35, kwa mujibu wa  Marca .

MAN UTD YAMWANDALIA DAU BARTRA


Marc Bartra Borussia Dortmund
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili beki mahiri wa Borussia Dortmund Marc Bartra, kwa mujibu wa  AS .
Mourinho tayari ameshakiimarisha kikosi chake katika safu ya ulinzi kwa kumsajili Victor Lindelof kutoka Benfica na anaamini beki wa zamani wa Barcelona Bartra ataongeza chachu kwenye kikosi chake.

CHELSEA YAANDAA DAU KWA AJILI YA ALLI


Dele Alli, Tottenham
Chelsea wamejipanga kutoa dau nono la rekodi kwa ajili ya kiungo wa Tottenham Dele Alli, kwa mujibu wa Don Balon .
Antonio Conte anataka kufanya makubwa katika dirisha la uhamisho wa majira ya joto, na anataka kumnunua Dele Alli licha ya bei yaku kutajwa kuwa euro milioni 100.

MAHREZ KUUNGANA NA ARSENAL


Riyad Mahrez Leicester City
Arsenal wapo mbioni kutangaza usajili wa winga wa Leicester City Riyad Mahrez ndani ya siku chache zijazo, limeripoti Calciomercato .
Mahrez amekuwa akitafuta kuondoka Leicester majira ya joto na kwa mujibu wa habri alikuwa akisubiri ofa kutoka Barcelona.
Hata hivyo baada ya kuona hakuna ofa yoyote kutoka Barcelona, Mahrez sasa anatarajiwa kujiunga na Arsenal, akiwa bado anahusishwa na tetesi za kutaka kutimkia Chelsea.

CHELSEA YAZUNGUMZA ZAIDI NA ALEX SANDRO


Alex Sandro Juventus
Chelsea itafanya mazungumzo zaidi Jumatatu katika harakati zao kumsajili beki wa Juventus Alex Sandro kwa dau la rekodi la klabu kwa paundi milioni 60, kimeripoti  The Telegraph .

DEPOR WANATARAJI KUKAMILISHA DILI LA PEREZ


Lucas Perez Arsenal
Deportivo La Coruna wanatuami Arsenal watapunguza dau wanalolitaka ili kumwachilia mshambuliaji wao Lucas Perez, kwa mujibu wa AS .
Arsenal wapo tayari kumuuza Perez, lakini bado hawajapokea ofa yoyote kwa ajili ya mchezaji hyo. Depor wanatamani Arsenal wakubali kumuuza Perez kwa kiasi kidogo kisichozidi euro milioni 12.

MOURINHO ANATAKA KUBAKI NA DARMIAN


Matteo Darmian Manchester United
Jose Mourinho anataka Matteo Darmian abaki Manchester United msimu ujao lakini mchezaji huyo anahitaji kuondoka iwapo atapata klabu ya Italia majira ya joto, kwa mujibu wa  ESPN .
Darmian ametajwa kuwa kwenye rada za Juventus na Inter kufuatia ripoti kuwa anataka timu itakayompa muda zaidi wa kucheza ili apate nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwakani.

MAN UTD YAMTOLEA MACHO LUKAKU


Romelu Lukaku Everton
Manchester United inataka kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton, hata kama watafanikiwa kumsajili Alvaro Morata, limeripoti gazeti la The Sun .
United wanatarajia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Real Madrid, lakini Jose Mourinho anataka kusajili washambuliaji wawili majira ya joto na Lukaku ni moja ya shabaha zake.

LIVERPOOL YAMZUIA STURRIDGE KUONDOKA


Daniel Sturridge Liverpool
Daniel Sturridge hataruhusiwa kuondoka Liverpool majira ya joto kwa sababu wanaamini itawagharimu fedha nyingi kupata mbadala wake, kwa mujibu wa Sunday Mirror .
Paris Saint-Germain na West Ham zimekuwa zikiifukuzia saini ya Sturridge, ila ofa kubwa tu itaweza kumshawishi Jurgen Klopp kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza.

HART ARUHUSIWA KUJIUNGA NA MAN UTD


Joe Hart England
Pep Guardiola atamruhusu Joe Hart kujiunga na Manchester United kutokea Manchester City msimu huu wa majira ya joto, limeripoti  Daily Express .
United watahitaji kusajili kipa mpya ikiwa David De Gea ataimkia Real Madrid majira ya joto na Hart anakaridiwa kuwa na thamani ya £25 millioni.

ALEXIS AMEZUILIWA KUJIUNGA NA MAN CITY


Alexis Sanchez Chile
Arsenal haitamruhusu Alexis Sanchez kujiunga na Manchester City majira ya joto, kwa mujibu wa  Daily Mail .
Washika Mtutu hao wa London hawataki kuwapa silaha wapinzani wao, na badala yake watamruhusu Alexis kujiunga na klabu za nje ya nchi, PSG wakipewa nafasi kubwa kumsajili.

EVERTON YAMTENGEA £20M GIROUD


Olivier Giroud Arsenal
Everton wanataka kutoa dau la paundi 20 millioni kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, limeripoti gazeti la  The Sun .
West Ham na Marseille zinatamani kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa lakini Everton wapo katika nafasi nzuri zaidi kumsajili.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages