Tetesi za usajili asubuhi ya leo july 2. 2017.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 2 July 2017

Tetesi za usajili asubuhi ya leo july 2. 2017..


Arsene Wenger anajiandaa kuvunja rekodi ya uhamisho ya dunia kwa kutoa dau la pauni milioni 125 kumnasa kinda wa Monaco, Kylian Mbappe.

Kocha Jurgen Klopp amemzuia mshambuliaji Daniel Sturridge kuondoka Liverpool kwa madai itawagharimu sana kuziba pengo lake.


Wayne Rooney ameaimbia Manchester United kuwa hawezi kung’atuka klabuni bila kulipwa dau la pauni milioni 30 kama ‘mkono wa kwaheri’.

Newcastle United inamtaka mshambuliaji Cedric Bakambu lakini italazimika kuvunja rekodi yake ya dau la uhamisho kumnasa kutoka Villarreal.

Newcastle United imeungana na West Ham na Watford katika mbio za kumtaka kipa asiyetakiwa Manchester City, Joe Hart.

Celtic inataka kuipa Chelsea pauni milioni 4.5 kupata saini ya chipukizi Charly Musonda

No comments:

Post Bottom Ad

Pages