Tetesi za Usajili Arsenal leo jumatatu ya july 03. 2017.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 3 July 2017

Tetesi za Usajili Arsenal leo jumatatu ya july 03. 2017..Imethibitika sasa kuwa mazungumzo yamefikia hatua nzuri baina yao na Arsenal na uhamisho unaweza kukamilika muda wowote

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amebanisha kuwa Arsenal wanaweza kumsajili rasmi mshambuliaji nyota Alexandre Lacazette ndani ya siku mbili kwa dau la kuvunja rekodi.

Washika Mtutu hao wa London wamemfanya mchezaji huyo wa Kimataifa wa Ufaransa kuwa kipaumbele chao nambari moja kuelekea kampeni za msimu mpya na wamejipanga kulipa paundi milioni 44 ikiwa ni paundi milioni 6 zaidi ya zile walizoilipa Real Madrid kumsajili Mesut Ozil miaka minne iliyopita.

Aulas alionekana kupotezea habari hizo Jumapili mchana kwamba usajili huo ulikuwa karibu kukamilika, akikanusha ripoti kwa vyanzo vya Ufaransa kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ametua Uingereza kwa vipimo vya afya.

Wakala wa Hector Bellerin anashughulikia uhamisho kurudi Barcelona

Hata hivyo, imethibitika sasa kuwa mazungumzo yamefikia hatua nzuri baina yao na Arsenal na uhamisho unaweza kukamilika muda wowote, lakini kiasi kitakacholipwa kwa ajili ya mshambuliaji huyo hakijawekwa bayana.

"Uhamisho wa Alexandre Lacazette kwenda Arsenal unaweza kukamilika ndani ya siku moja au mbili," alikiambia Le Progres . "Tunaweza kufikia rekodi mpya - si usajili mdogo, euro milioni 50 kwa mchezaji anayetoka kwenye klabu yetu.

Fuatilia tetesi za uhamisho Majuu hapa

"Ofa ya kwanza kufanywa na Arsenal ilikuwa euro milioni 45.Dili linaweza kuwa na thamani kati ya euro 45 na 50 milioni. Euro milioni 67 zilizotangazwa na vyanzo vya Uingereza ni uongo na jambo lisilowezekana, si hesabu ya ukweli."

Lacazette alikuwa ameelekeza macho yake kujiunga na Atletico Madrid majira ya joto, lakini kufungiwa kwa klabu hiyo kufanya usajili kulizima ndoto yake hiyo.

Mchezaji huyo aliyekuwa shabaha ya West Ham United amefunga mabao 129 katika mechi 275 kwa klabu ya Lyon, ambapo 37 yalipatikana katika kampeni za 2016-17.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages