Stars yaionyesha shughuli Afrika kusini, yatinga nusufainali. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 2 July 2017

Stars yaionyesha shughuli Afrika kusini, yatinga nusufainali.


Tinu ya taifa ya Tanzania imefuzu hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wa michuano hiyo ya COSAFA Afrika ya kusini.

Stars imepata ushindi huo kwa goli pekee la mshambuliaji wake anakipiga huko Uarabuni Elias Maguli. Maguli amefunga goli hilo mnamo dakika ya 18 baada ya kujikunjua na kuachia shuti safi lililomshinda mlinda mlango wa Afrika ya kusini ,goli lililodumu hadi kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa mashambulizi ya hapa na pale huku stars ikioneka kana kuzidiwa hasa dakika 20 za mwisho za kipindi cha pili kilichopekea kuzongwa sana katika lango lake licha ya kua haikuwadhuru.
Afrika ya kusini watajilaumu kwa kuweka dharau kwa Stars ambayo imekwenda huku ikiwa na malengo mawili ambapo la kwanza ikiwa ni kuhakikisha inasonga mbele na la pili ikiwa ni kulipiza kisasi kwa timu hiyo ya Afrika ya kusini kwa kipigo cha mwaka uliopita.
Sasa Tanzania  Itakutana na Zambia katika mchezo wa nusu faina.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages