Singida United yamnyakua mshambuliaji kutoka Simba huyu hapa. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 5 July 2017

Singida United yamnyakua mshambuliaji kutoka Simba huyu hapa.


Mshambualiaji Pastory Athanas amejiunga na wageni wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Singida United kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea kwa Mabingwa wa Kombe la Azam Sports Federation Simba SC. 
Pastory alijiunga na Simba mwishoni mwa Mwaka Jana akitokea Stand United na hiyo ni baada ya Kuwafunga Azam na Yanga akiwa Stand United. 
Alipokuwa Simba. 
Tangu alipojiunga na Simba SC amefunga bao moja pekee bao ambalo alilipata katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 Bora dhidi ya Polisi Dar. 
Tayari klabu ya Singida United kupitia kwa Mkurugenzi wao Festo Sanga wamethibitisha kuinasa Saini ya Mshambualiaji huyo ambaye wanamtaja kuwa ataleta upinzani kwenye safu ya ushambuliaji. 
-Pastrory Athanas ni moja ya wachezaji wazuri ambao ni vijana Lakini hakuwa chaguo la Kocha Joseph Omog na ameona aje kutuhudumia sisi, amesajiliwa kwa kandarasi ya miaka miwili" Ilisema sehemu ya taarifa hiyo. 
Kujiunga Kwa Pastory kunaifanya Singida United kuwa na wachezaji wengi eneo la ushambuliaji Kama Atupele Green, Mrwanda Danny Usengimana, Mzimbabwe Nhivi Simbarashe.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages