Singida United kama kawaida yamnasa mwingine wa kimataifa kutoka Rwanda. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 11 July 2017

Singida United kama kawaida yamnasa mwingine wa kimataifa kutoka Rwanda.


Klabu ya Singida United imekamalisha Usajili wa wachezaji wa Kimataifa baada ya Hii Leo kufikisha Idadi ya wachezaji Saba wanaohitajika Kwa Mujibu wa Kanuni za ligi Kuu Soka Tanzania Bara.
Singida United imekamalisha Usajili wa Beki wa Timu ya Taifa ya Rwanda na Nahodha wa APR Michel Rusheshangoga. 
Michel ambaye ametwaa tuzo ya Bao bora la msimu kwa ligi kuu ya Rwanda ametua nchini na kwenda moja kwa moja kuungana na wenzake walipo kambini Jijini Mwanza.

Danny Usengimana. 
Vilevile klabu hiyo imemtambulisha rasmi mfungaji bora wa misimu miwili mfululizo Ligi kuu ya Rwanda, Danny Usengimana, Mchezaji huyo ambaye ni tegemeo kwa timu ya Taifa ya Rwanda ameingia mkataba wa kuitumikia Singida United kwa miaka miwili. 
Wachezaji wengine wa kimataifa wa Singida United ni pamoja na Elisha Muroiwa,Wisdom Mutasa, Raphael Kutinyu, Simbarashe 'Simba' Nhivi Sithole, pamoja na Shafik Batambuze. 
Singida United ipo Jijini Mwanza, kwa ajili ya kambi maalumu ya kuimarisha kikosi tayari kwa mapambano ya Ligi kuu msimu wa 2017/2018 Tanzania bara.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages