Simba kuwatema hawa hapa msimu ujao. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 3 July 2017

Simba kuwatema hawa hapa msimu ujao.


Wachezaji nyota wa Simba Jamvier Bukungu, Juuko Murshid na Fredrick Blagnon, huenda wasiwepo kwenye kikosi cha mabingwa wa Kombe la FA, kutokana na viwango vyao kushuka na kushindwa kuendana na mahitaji ya timu.

Imani Kajuna ambaye amepewa nafasi ya kukaimu nafasi ya Urais wa klabu hiyo ameiambia Goal, kwa sasa wanaandalia wachezaji hao barua za kuwataarifu huko walipo ili waanze taratibu za kusaka timu za kujiunga nazo kabnla kipindi cha usajili hakijapita.

“Nikweli Kamati yetu imepanga kuachana na wachezaji hao na hiyo imetokana na usajili ambao tumeufanya kwamfano wa beki wa kulia tumemsajili Shomari Kapombe na Ally Shomar hapo utaona kuwa Bokungu, hana nafasi lakini pia kuna mshambuliaji tunatarajia kumtangaza hivi karibuni atakaye ziba nafasi ya Blagnon pamoja na beki wa kati,” amesema Kajuna.

Kiongozi huyo  amesema mbali na nyota hao wakigeni pia kuna baadhi ya wachezaji wazalendo wanatarajia kuwatupia virago baada ya mchango wao kuwa mdogo na kushindwa kufikia malengo ya timu.

Wachezaji hao ni beki wa kulia Juma Hamad , Pastory Athanas, Jamali Mnyate  na Novaty Lufunga ambao wamepewa ruhusu ya kutafuta timu za kuchezea msimu ujao na wengine wamemaliza mikataba yao .

Kajuna amesema hivi sasa asilimia kubwa ya mambo yao kuhusiana na usajili yanakwenda sawa na wanaamini hakuna kitakacho habaribika hadi wakati ambapo msimu mpya wa ligi ya Vodacom utakapoanza.

“Niwaambia mashabiki na Wanachama wa Simba tuwe watulivu kwa kipindi hiki ambacho tupo kwenye maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya, lakini pia wakati huo tunapambana kuhakikisha viongozi wetu wanarudi uraiani na kuendelea na majukumu yao kama ilivyokuwa zamani,” amesema Kajuna.

Uongozi wa Simba kwasasa upo katika mikakati ya kumwongezea mkataba kiungo wake mkabaji raia wa Ghana James Kotei , ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake wa miezi sita aliosajiliwa kwenye dirisha dogo la msimu uliopita.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages