Samatta huyoo na Everton - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 11 July 2017

Samatta huyoo na EvertonLICHA ya timu za Tanzania kukosa nafasi ya kuikabili timu ya Everton inayoshiriki Ligi Kuu ya England, straika Mbwana Samatta, yeye amepata fursa hiyo.

Kulingana na ratiba ya timu hiyo, baada ya msafara wa Everton kumaliza ziara yake nchini Tanzania, utaelekea nchini Ubelgiji na kucheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya KR Genk ambayo Samatta anaichezea.

Kikosi cha Everton kinatarajia kutua nchini Julai 12, kwa ajili ya ziara maalumu ya kimichezo ambapo inatarajia kucheza mechi moja dhidi ya timu ya Gor Mahia ya Kenya ambayo imepata fursa hiyo baada ya kuibuka  mabingwa wa michuano ya Sport Pesa.

Michuano ya Sport Pesa iliyofanyika nchini majuma kadhaa yaliyopita, ilishirikisha timu nane kati ya hizo nne kutoka Tanzania na nyingine nne kutoka Kenya.

Samatta ameendelea kuwa mchezaji mwenye mafanikio makubwa kupitia soka lake, kwani mbali na hilo amechaguliwa kuwa balozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages