Sakata la malinzi kughalimu zaidi ya Dola 514,618 - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 1 July 2017

Sakata la malinzi kughalimu zaidi ya Dola 514,618RAIS wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, anatuhumiwa kughushi nyaraka mbalimbali ndani ya shirikisho hilo pamoja na kutakatisha pesa ambazo jumla yake ni Dola 514,618   zaidi ya Sh 1.1 bilioni.

Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Celestine Mwesigwe, juzi Alhamisi walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa makosa yao ambapo Malinzi alikuwa na makosa 28 huku Mwesigwa na Mkurugenzi wa Fedha wa TFF, Nsiande Mwanga, wakiwa na makosa matatu kila mmoja.

Malinzi na wenzake walishindwa kuwekewa dhamana kutokana na kesi yao ilivyo ambapo kisheria tuhuma za utakatishaji pesa hazina dhamana kwa mujibu wa kanuni ya 148 (5). Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri, aliahirisha kesi hiyo hadi keshokutwa Jumatatu, Julai 3, ambapo atatoa uamuzi kama washitakiwa watapata dhamana ama wataendelea kukaa rumande. Makosa anayotuhumiwa kukutwa nayo Malinzi ni haya.

Shitaka la kwanza

Juni 5, 2016, Dar es Salaam, Malinzi na Mwesigwa walihusika kughushi nyaraka zinazoitwa maazimio ya Kamati ya Utendaji (Executive Committee Resolution) za Juni 5, 2016 wakionyesha Kamati ya Utendaji ya TFF imebadili mtia saini wa akaunti ya benki ya shirikisho hilo, Edgar Leonard Masoud na badala yake awe Nsiande Isawafo Mwanga wakati wakijua si kweli.

Shitaka la pili,

Septemba

Mosi, 2016

Mwesigwa aliwasilisha nyaraka zilizoghushiwa benki ya Stanbic tawi la Kinondoni, nyaraka hiyo ya kughushi inayoonyesha Kamati ya Utendaji ya TFF imebadili mtia saini huyo.

Shitaka tatu,

Desemba 17, 2013

Malinzi alighushi stakabadhi namba 308 ya Novemba 6, 2013 akionyesha kuikpesha TFF dola 9,300 (Sh 19 milioni).

Shitaka la nne, Disemba 17, 2013

Malinzi alidaiwa katika ofisi ya TFF, alighushi risiti namba 322 akionyesha ameikopesha TFF dola 10,000 (Sh 20 milioni).

Shtaka la tano, Desemba 17, 2013

Malinzi anadaiwa alighushi risiti namba 323, akionyesha ameikopesha TFF dola 18,000 (Sh37 milioni).

Shita la sita,

Desemba 17, 2013,

Malinzi alighushi risiti namba 324 akionyesha ameikopesha TFF Dola 500 (Sh1.2 milioni).

Shtaka la saba,

Desemba 17, 2013

Malinzi anadaiwa katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba 325 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,032(Sh2.1 milioni).

Shitaka la nane,

Machi 26,2014

Katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1956 akionyesha ameikopesha TFF dola 40,000 (Sh84 milioni).

Shitaka la tisa,

Machi 13, 2014

Malinzi alighushi risiti namba 1957 akionyesha ameikopesha TFF dola 5000 (Sh 10 milioni).

Shitaka la 10,

Mei 13, 2014

Inadaiwa kuwa katika ofisi ya TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1624 akionyesha ameikopesha TFF dola 40,000( Sh 84 milioni).

Shitaka la 11,

Mei 16, 2014

Malinzi anadaiwa alighushi risiti namba 1634 akionyesha ameikopesha TFF dola 10,000 (Sh 20 milioni).

Shitaka la 12,

Julai 11, 2014

Ilielezwa kuwa katika ofisi hiyo ya TFF alighushi risiti namba 1860 akionyesha ameikopesha TFF dola 15,000 (Sh 30 milioni).

Shitaka la 13,

Julai 11, 2014

Katika ofisi hiyo ya TFF alighushi risiti namba 1861 akionyesha ameikopesha TFF dola 3,000( Sh 6 milioni).

Shitaka la 14,

Julai 15, 2014

Malinzi alighushi risiti namba 1863 kuwa ameikopesha TFF dola 14,000 (Sh 28 milioni).

Shitaka la 15,

Julai 15, 2014,

Inadaiwa kuwa Malinzi katika ofisi ya TFF alighushi risiti namba 1866 akionyesha ameikopesha TFF dola 4,000( Sh 8 milioni).

Shitaka la 16, Julai 25, 2014 Malinzi anadaiwa alighushi risiti namba 1876 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,000 (Sh 2.2 milioni).

Shitaka la 17,

Agosti 19, 2014,

Malinzi alighushi risiti namba 1890 akionyesha ameikopesha TFF Dola 5000 (Sh10 milioni).

Shitaka la 18,

Oktoba 11, 2014

Kwenye ofisi hizo za TFF, Malinzi alighushi risiti namba 1568 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,200 (Sh2.4 milioni).

Shitaka la 19,

Agosti 17,2015

Malinzi anadaiwa kuwa kwenye ofisi hiyo ya TFF alikula njama ya kughushi risiti namba 1511 akionyesha ameikopesha TFF dola 5,000 (Sh10 milioni).

Shitaka la 20,

Julai 22, 2015

Kwenye ofisi za TFF, Malinzi alighushi risiti namba 2981 akionyesha ameikopesha TFF dola 2,000 (Sh 4 milioni).

Shitaka la 21

alidai kuwa Mei 9,2016,

Malinzi alighushi risiti namba 832 akionyesha ameikopesha TFF dola 7,000 (Sh 14 milioni).

Shtaka la 22,

Juni 16, 2016,

Malinzi alighushi risiti namba 931 akionyesha ameikopesha TFF dola 10,000 ( Sh 20 milioni).

Shitaka la 23,

Agosti 2, 2016,

Malinzi alighushi risiti namb 947 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,000 (Sh2.2 milioni).

Shitaka la 24,

Septemba 19, 2016,

Malinzi alighushi risiti namba 1029 akionyesha ameikopesha TFF dola 1,000( Sh 2 milioni).

Shitaka la 25,

Septemba 22, 2016,

Malinzi alikula njama ya kughushi risiti namba 1071 akionyesha ameikopesha TFF dola 15,000 (Sh 30 milioni).

Shitaka la 26, kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19, 2016

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande kwa pamoja na kwa kushirikiana walitakatisha fedha kiasi cha dola 375,418 (Sh840 milioni).

Shitaka la 27, Septemba Mosi na Oktoba 19,2016

Malinzi na Mwesigwa katika kipindi hicho katika benki ya Stanbic tawi la kati la Kinondoni walijipatia dola 375,418 wakati wakijua fedha hizo zimetokana na kughushi.

Shitaka la 28, kati ya Septemba Mosi na Oktoba 19,2016

Mshtakiwa Nsiande anadaiwa kati ya kipindi hicho katika ofisi ya TFF alimsaidia Malinzi na Mwesigwa kujipatia dola 375,418 kutoka benki ya Stanbic huku akijua upatikanaji wake umetokana na kughushi.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages