Pogba ampongeza Lukaku - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 8 July 2017

Pogba ampongeza LukakuNa Yego Shola
Paul Pogba amempongeza mchezaji mwenzake mpya Romelu Lukaku kwa uhamisho wake wa kutua Manchester United.

Kiungo huyo wa United yupo mapumzikoni akiwa na Lukaku jijini Los Angeles ambako straika wa Kibeligiji Lukaku anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya huko na kukamilisha maslahi yake binafsi ambapo United wanatarajiwa kutua nchini Marekani hiyo kesho kwa maandalizi ya msimu mpya.

Pogba alitengeneza video fupi ya ujumbe wa kumkaribisha Lukaku kupitia Instagram leo Jumamosi ambayo inasema," Tutaonana kesho mazoezini" baada ya Manchester United kuthibitisha mapema kwamba wamekubali dili la kumsajili Lukaku.

Akiongea kwa Kifaransa Lukaku amesema," Ilikuwa kazi, tumeifanikisha, tunamkutano kesho ." Pogba nae akajibu ," umesemaje ?" Lukaku akajibu," Mkutano kesho, unaweza kuamini ?" Pogba akapiga kelele," Ndio mkuu "

Taarifa kutoka Sky Sports zinasema kwamba United watalipa kiasi cha pauni milioni 75 pamoja na ongezeko la pauni milioni 15 katika kipindi cha mkataba wake na Man United na Wayne Rooney atahamia Goodison Park.

Na United walionyesha wamempata mtu wao licha ya Sky Sports kuarifu kwamba Chelsea wameingilia kati jana Ijumaa usiku ambapo waliwaambia Everton kwamba wapo tayari kufikia ofa ya United.

Pogba na Lukaku walikuwa wakifanya mazoezi pamoja katika viwanja vya UCLA, na wanatumia wakala mmoja Mino Raiola.

Mahusiano mazuri sana ya Raiola na United pamoja na Mourinho yamewasaidia kumnasa mchezaji ambaye  Chelsea walikuwa wanamuhitaji kuwa chaguo lao namba moja.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages