Picha: Hivi ndivyo mchezo kati ya Lesotho na Tanzania ulivyokua - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 7 July 2017

Picha: Hivi ndivyo mchezo kati ya Lesotho na Tanzania ulivyokua


Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania 'Taifa Stars' imefanikiwa kuchukua nafasi ya tatu ya michuano ya COSAFA Castle Cup baada ya Kuwafunga Lesotho. 


Licha ya Tanzania kushindwa Kuwafunga Lesotho katika dakika 90 za mchezo lakini ni mikwaju ya penati Ndio iliyoamua mchezo huo baada ya kutoka Suluhu ya 0-0.


Dakika ya pili tu Lesotho walionesha kuwa walikuwa wakihitaji ushindi Kwani Mpira wa Kichwa uliopigwa na Sera ulishindwa kuzama Wavuni baada ya kudakwa na Kipa Said Mohammed.
Aidha dakika ya Sita Tanzania walipanda mbele kwa Kasi na kuanzisha mashambulizi Lakini umakini wa Stamil Mbonde ulikosekana na kujikuta Anapokea Mpira akiwa eneo la kuotea.
Dakika zote 45 za kipindi cha kwanza Lesotho walikuwa bora zaidi ya Tanzania wakikosa nafasi nyingi za wazi pamoja na kujenga makazi langoni mwa Tanzania.

Kipindi cha pili. 
Kipindi cha pili kilianza kwa Tanzania kuendelea kucheza hovyo, Huku ukuta wao ukikatika Mara Kwa mara na kuruhusu mashambulizi Lakini Uimara wa Mlinda Mlango Said Mohammed ukaendelea kuwa Mwiba mchungu kwa Lesotho.
Kocha Shaban Salumu Mayanga alifanya mabadilko kwa kuwatoa Salimu Mbonde, Salmini Hoza na Stamil Mbonde na kuwaingiza Elias Maguri, Mzamiru Yasini Na Abdi Banda Lakini mabadiliko hayo hayakusaidia chochote Kwani hadi dakika 90 zinamalizika Tanzania 0-0 Lesotho. 
Penati
Timu zikaingia katika Mikwaju ya penati ili Kuamua Mshindi katika mchezo huo ambapo Tanzania walipata nne Na Lesotho wakapata penati Mbili. 
Waliopiga penati kwa upande wa Tanzania ni Shizya Ramadhan Kichuya Aliyekosa Huku Himid Mao Mkami, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Daudi wakifanikiwa Kukwamisha Mipira nyavuni.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages