Mtibwa Sugar kusalia na kocha wake mkuu kwa msimu mwingine zaidi. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 11 July 2017

Mtibwa Sugar kusalia na kocha wake mkuu kwa msimu mwingine zaidi.Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar imethibitisha wazi kuwa Msimu ujao Itaendelea kuwa Kocha Zuberi Katwila kama Kocha Mkuu wa Timu hiyo huku Kocha wa Partick Mwangata akiwa kocha Msaidizi.
Kauli hiyo inatoka wakati ambapo Kocha wa Zamani wa Kagera Sugar Rishald Adofl akiwa anahusishwa na kujiunga na mabingwa hao wa taji la Ligi kuu Bara Mwaka 2000 kama Kocha wao Mkuu toka alipoondoka Salumu Shaban Mayanga aliyejiunga na Timu ya Taifa.
Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru Ligalambwike ameweka wazi kuwa Zuberi Katwila ataendelea kuwa kocha wao kwa Msimu ujao wa Ligi na hakuna mabadiliko yoyote ambayo yatafanywa katika Benchi la Ufundi kwa siku za Hivi karibuni.
Tutakuwa naye Msimu ujao.
-Ninachofahamu baada ya kuondoka kwa Salumu Mayanga, Zuberi Katwila aliyekuwa kocha Msaidizi aliichukua Timu na ndiye ambaye anaiongoza Mtibwa mpaka sasa na hakika niseme tu kwamba ataendelea kuwa Kocha Mkuu katika Msimu ujao wa Ligi ya Vodacom”
Kifaru amesema hata Timu ya sasa Inajengwa kwa Karibu zaidi na Zuberi Katwila ambaye ndiye anayesuka Mipango yote kuhakikisha kwamba Mtibwa Sugar inakuwa Moto wa Kuotea Mbali Msimu Ujao.
Kambi ya Msimu ujao.
Wakati huohuo Kikosi hicho cha Mtibwa Sugar kinatarajia kuanza Kambi ya Msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara Jumatano ya wiki hii, Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Thobias Kifaru ni kwamba kambi hiyo itaenda Sambamba na Mazoezi magumu na ya kiufundi kwa wachezaji wote ambao tayari wamejiunga na Kikosi hicho  na kwamba Kambi hiyo itachukua muda wa Takribani Majuma Mawili.
Kifaru amesema mara baada ya Kukamilisha Kambi hiyo watasafiri Hadi Mkoani Morogoro ambapo wakiwa hapo watacheza mchezo mmoja wa Kirafiki na Timu ya Kizazi Kipya Mbeya City kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages