Mtibwa kambini kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu msimu wa 2017/2018 - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 10 July 2017

Mtibwa kambini kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu msimu wa 2017/2018Mtibwa Sugar itapiga kambi ya wiki mbili jijini Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara utakaoanza mwishoni mwa Agosti.
Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema kambi hiyo itaanza Jumatano na wanaamini itawasaidia kufanya vizuri kwenye msimu ujao wa ligi.
 Kifaru alisema kwa asilimia kubwa wamemaliza usajili wao mabao wameufanya kwa umakini hasa kwa kusajili vijana ambao wanaamini wataipa mafanikio klabu hiyo.
Alisema baada ya wachezaji kadhaa kuondoka katika timu hiyo akiwemo beki Salim Mbonde na winga Ally Shomari waliotimkia Simba wamewaongeza wachezaji vijana kuziba nafasi zao wakiwemo Hassan Iddi kutoka  Oljoro JKT na  Salum Ramadhan  kutoka Polisi Morogoro.
"Tutaweka kambi ya mazoezi kwa wiki mbili Dar es Salaam  mpaka Julai 28  na Julai 29 tutacheza mchezo wa kuwania kombe la  Faith Baptist  dhidi ya Mbeya City  utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri  Morogoro na baada ya mchezo huo tutarejea Turiani kuendelea na kambi,"alisema Kifaru.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages