Messi: Sio wa Yanga Wala Simba ,huyooo atimkia kwenye klabu hii - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 15 July 2017

Messi: Sio wa Yanga Wala Simba ,huyooo atimkia kwenye klabu hii

Ungana nasi kila siku kwa habari mbalimbali za michezo kitaifa na kimataifa ,tetesi mbalimbali za Usajili bila kusahau magazeti kila siku kwa kudownload application yetu leo.BOFYA HAPA KKUDOWNLDKiungo mshambuliaji wa Azam Fc Ramadhani Singano huenda akaachana na timu hiyo na kujiunga na Difaa Al Jadida ya Morocco.
Singano ameiambia Goal, mpaka kufikia sasa mazungumzo yao yapo katika dakika za mwisho ili aweze kusaini kuichezea timu hiyo ambayo imemhaidi dau nono.
“Ni kweli mungu akipenda huenda nikaondoka Azam na kujiunga na Al Jadida, kila kitu kinakwenda sawa na baada ya siku chache naweza kuondoka nchini kwa ajili ya kuanza kazi rasmi,”amesema Singano.
Kiungo huyo amesema kinachomuondoa Azam ni maslahi mazuri ambayo ameahidiwa huko na anamuomba mungu mipango hiyo isivurugike ili aweze kutimiza malengo yake ya kucheza soka la kulipwa nje yaTanzania.
Amesema anatambua changamoto zilizopo kucheza nje ya nyumbani lakini soka ndiyo kazi yake hivyo hawezi kukataa ofa kama hiyo aliyoahidiwa.
“Najua soka la wenzetu limepiga hatua sana lakini kama mchezaji nahitaji changamoto kama hizo kwasababu zinanijenga na kuniongezea ari ya kufanya vizuri siku hadi siku,”amesema .
Msimu uliopita, Al Jajida ilishika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Morocco maarufu kama Botola nyuma ya mabingwa, Raja Casablanca. Maana yake itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages