Mayanga awaogopa Afrika Kusini, kutibua rekodi yake. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 1 July 2017

Mayanga awaogopa Afrika Kusini, kutibua rekodi yake.Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania 'Taifa Stars' Salumu Shabani Mayanga amewaelezea wapinzani wao katika mchezo wa Robo fainali ya Michuano ya Baraza la soka kwa nchi za kusini mwa Afrika (COSAFA) kuwa sio wa kubeza.

Mayanga amesema wanajua wazi kuwa wanaenda kuumana na Afrika Kusini ambao ndio wenyeji wa Michuano hiyo lakini watahakikisha wanatumia kila mbinu ili kuibuka na ushindi na hatimaye kusonga mbele.

-Tunajua wazi kuwa tunaenda kucheza na Timu Ngumu ya Afrika Kusini, tulitambua hilo mwanzo kabisa wa michuano, Afrika kusini sio wabaya ni Timu nzuri sana najua watatoa upinzani wa kweli lakini na sisi tumejipanga kuhakikisha tunatoa upinzani na kuibuka na ushindi' Alieleza Mayanga.

Tanzania wanatajia kucheza na Afrika Kusini katika Mchezo wa Robo Fainali Jumapili ya Julai Mosi na hiyo ni baada ya kuongoza kundi A wakiwa na alama 5 baada ya kushinda mchezo Mmoja dhidi ya Malawi na Kutoka sare dhidi ya Angola na Mauritius.

Rekodi ya Mayanga.
Aidha kwa upande wa Kocha anaingia katika mchezo huo akiwa na rekodi ya kipekee ya kutopoteza katika michezo Sita akishinda Michezo Mitatu na Kutoka sare michezo Mitatu.

Alianza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Botswana, akashinda 2-1 dhidi ya Burundi, akatoka sare ya 1-1 na Lesotho, baada ya hapo akawafunga Malawi 2-0, akatoka sare 0-0 na Angola na mwisho alitoka sare ya 1-1 na Mauritius.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages