Matokeo COSAFA :Lesotho vs Tanzania. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 7 July 2017

Matokeo COSAFA :Lesotho vs Tanzania.Dakika 90' za mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu wa michuano ya COSAFA kati ya waalikwa wa mashindano hayo Tanzania dhidi ya timu ya taifa ya Lesotho zimemalizika kwa timu hizo kutoka sare tasa ya bila kufungana huku mda huu timu zote zikiingia katika hatua ya matuta.


Mpira umekwisha kwa timu ya taifa ya Tanzania kuibuka kidedea kwa mikwaju ya penati kwa penati 4-2 baada ya timu ya taifa ya Lesotho kukosa penati 2 huku Tanzania ikikosa penati moja iliyopigwa na Shiza Ramadhani Kichuya.


Katika mchezo huo Lesotho imeongoza kwa kupiga mipira yenye malengo 13 huku mipira 7 kati ya hiyo ikilenga langoni moja kwa moja na Tanzania kupiga mipira 5 huku 2 kati ya hiyo ikilenga golini.
Hakuna faulo hata moja iliyopigwa wakati kona zikipigwa 2-2.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages