Malinzi ajiuzulu nafasi yake FIFA - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 8 July 2017

Malinzi ajiuzulu nafasi yake FIFARais wa Shirikisho la Soka nchini 'TFF', Jamal Malinzi amejiuzulu wadhifa wake wa Ujumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Shirikisho la Soka la Ulimwengu 'FIFA' Nafasi ambayo ameitumikia Tangu Januari mwaka huu.
 Taarifa hiyo ni Kupitia kwa wakili wake, kutoka kampuni ya Rwegoshora, ambayo imethibitisha kuwa Malinzi amewaandikia barua FIFA kuwataarifu kujitoa kwenye Kamati hiyo kutokana na kuwa mikononi mwa dola kwa sasa. 
 Aidha alipotafutwa Kaimu Rais wa TFF Wallace Karia kuthibitisha taarifa hizo alikuwa Kimya hadi pale baadae aliposema kuwa suala hilo halipo katika Ofisi yake kwa sasa. 
 Malinzi, pamoja na Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu Nsiande Isawafo Mwanga, wapo rumande hadi Julai 17, ambapo kesi yao ya Matumizi mabaya ya Ofisi na uhujumu uchumi itakapotajwa Tena.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages