Mabeki wa kati waliofanya vizuri ligi kuu Tanzania msimu uliopita. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 3 July 2017

Mabeki wa kati waliofanya vizuri ligi kuu Tanzania msimu uliopita.


Safu bora ya ulinzi ndiyo uti wa mgongo kwa klabu yeyote ile, mafanikio ya timu yeyote uchangiwa na uimara wa nguzo bora ya ulinzi.

Msimu uliopita kwenye Ligi Kuu safu ya ulinzi ilikuwa na changamoto kubwa sana kwa klabu nyingi, ndiyo maana mabeki wengi wamekuwa wakiingia na kutoka kwenye kikosi cha kwanza sababu kubwa ikiwa ni kushindwa kuwa na mwendelezo wa kiwango bora kila wiki.

Licha ya changamoto nyingi kwenye eneo hilo kuna baadhi ya mabeki walikuwa na kiwango bomba tangu mwanzoni mwa msimu.

Goal inakuletea mabeki waliofanya vizuri tangu mwanzoni mwa Ligi hadi mwisho kwa msimu uliomalizika.

Method Mwanjali (Simba)

Alikuwa na msimu mzuri ndani ya klabu ya Simba, uzoefu mkubwa kwa Mzimbabwe huyo kuliifanya Simba kuwa imara kwenye eneo la ulinzi, ana uwezo mkubwa kucheza mipira ya juu na kuanzisha mashambulizi vizuri.

Yakubu Mohammed (Azam)

Moja ya usajili bora kwa Azam msimu uliopita, Mohammed amefanikiwa kuziba pengo la Pascal Wawa kwa kiasi kikubwa, sifa yake kubwa ni kasi na matumizi ya nguvu aendapo kukaba.

Yusuph Ndikumana (Mbao Fc)

Kiraka wa klabu ya Mbao, Ndikumana ana uwezo wa kucheza namba 6,3,4 kwa ustadi mkubwa, mlinzi huyo amegeuka kiboko ya washambuliaji wanjanja na wenye kasi kwani amekuwa akiwazuia bila shida yeyote.

Salum Mbonde ( Mtibwa Sugar)

Ameendelea kuwa bora kwa misimu mitatu mfululizo, kiwango chake bora kimemfanya kurudishwa kwenye timu ya taifa chini ya mwalimu Mayanga, Mbonde ni mzuri kwa mipira ya hewani kutokana na kimo chake.

Nurdin Chona

Mlinzi wa Tanzania Prisons ya Mbeya, beki huyo ana uwezo mkubwa wa kuzuia mashambulizi ya kushutukiza sababu ana kasi na nguvu pia.

Asante Kwesi ( Mbao Fc)

Mghana wa klabu ya Mbao Fc, kiwango chake bora kwa msimu uliopita kimetokea kuwavutia klabu za Simba, Yanga na Azam kuiwinda saini yake kwa ajili ya msimu ujao, Kwesi amekuwa akitimiza majukumu yake ya ulinzi kwa asilimia kubwa

No comments:

Post Bottom Ad

Pages