Lwandamina Afunguka haya kuelekea mchezo kati ya Yanga na Simba - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 18 July 2017

Lwandamina Afunguka haya kuelekea mchezo kati ya Yanga na Simba

Ungana nasi kila siku kwa habari mbalimbali za michezo kitaifa na kimataifa ,tetesi mbalimbali za Usajili bila kusahau magazeti kila siku kwa kudownload application yetu leo.BOFYA HAPA KKUDOWNLD
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga George Lwandamina ameweka wazi msimamo wao na mtazamo wao kuelekea mchezo baina yao na watani wao wa jadi Simba Sc.

Kocha huyo amedai kuwa mechi dhidi ya Simba itawapa picha halisi na ndio kipimo watakachotumia kujipima sehemu waliyofikia baada ya kuanza mazoezi makali ya gym jijini Dar es Salaam. “Kikosi kinaendelea vizuri na mazoezi ya gym ili kujenga stamina ya wachezaji kwa sababu msimu ujao hauko mbali kuanza na tayari tunajua kuna ratiba ngumu ya kushiriki kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika,” alisema kocha huyo.


“Mechi yetu dhidi ya Simba hatuwezi kuibeza kama watu wanavyodhani, tutaingiza kikosi kamili kwa sababu tunataka kuitumia kupima uelekeo wetu, hivyo ushindi wa kila namna ndio mpango wetu namba moja,” aliongeza. “Najua namna ambavyo hizi mechi huwa zinachukuliwa na mashabiki na zimejaa kila aina ya hisia, hata sisi kama benchi la ufundi tunaheshimu hilo pia na ndio maana tumeanza maandalizi kwa nguvu zote,” alimaliza.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages