Kuondoka kwa Niyonzima Yanga kwamuumiza Ali kiba - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 8 July 2017

Kuondoka kwa Niyonzima Yanga kwamuumiza Ali kibaMkali wa Bongofleva Ali Kiba ni shabiki mkubwa Yanga na huwa hajifichi katika hilo huku mara kahaa akionekana uwanjani kuisapoti timu yake inapokuwa inacheza mechi mbalimbali.

Mbali na ushabiki wake wa Yanga, Ali Kiba na kiungo Haruna Niyonzima ni washkaji sana. Sasa Niyonzima ameondoka Yanga na haijafahamika hadi sasa anaelekea wapi ingawa anahusishwa kujiunga na Simba.

Kiba anazungumzia anavyojisikia baada ya uongozi wa Yanga kutangaza rasmi kwamba Niyonzima hata kuwa miongoni mwa wachezaji wao kuanzia msimu ujao.

“Nimejisikia vibaya kwa sababu mimi ni shabiki wa Yanga namkubali Niyonzima, lakini mpira ni kazi yake unapokuwa unatumikia sehemu kwa muda mrefu inafika kipindi unataka kwenda sehemu nyingine.”

“Kwanza ni historia nzuri kwake kwenye mpira kwamba amecheza klabu fulani na fulani, anatajwa kwenda Simba, ni klabu kubwa vilevile.”

“Nitaendelea kum-support kama mshkaji wangu lakini mimi ni shabiki wa Yanga na sija-mind yeye kutoka Yanga kwa sababu ni moja ya mafanikio kwake ameangalia maslahi na yeye ni mchezaji mpira.”

“Mchezaji mpira anafanana na sisi wanamuziki, tunaangalia panapokuwa na maslahi. Hata leo promota akiniambia ana kiasi hiki halafu mwingine akanipigia simu akaniambia ana zaidi nakwenda kwingine.”

“Vilevile sidhani kama amefanya maamuzi mabaya japokuwa mimi ni mwana Yanga na nilitamani aendelee kubaki Yanga ila ana uhuru.”

Niyonzima amewahi kuonekana mara kadhaa jukwaani kwenye show za Ali Kiba na wawili hao wamekuwa marafiki kwa muda mrefu sana.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages