Kocha Mayanga ataja sababu za kutoa sare na Rwanda - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 16 July 2017

Kocha Mayanga ataja sababu za kutoa sare na Rwanda

Ungana nasi kila siku kwa habari mbalimbali za michezo kitaifa na kimataifa ,tetesi mbalimbali za Usajili bila kusahau magazeti kila siku kwa kudownload application yetu leo.BOFYA HAPA KKUDOWNLD

Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga, amesema sababu ya kushindwa kufanya vizuri kwenye mchezo wa kwanza kuwania kufuzu fainali za CHAN dhidi ya Rwanda, kulitokana na uchovu waliokuwa nao wachezaji wake.
Mayanga ameiambia Goal, kuumia kwa beki wake wa kulia Shomari Kapombe ambaye alishindwa kuendelea na mchezo pia ilikuwa ni moja ya sababu ya wao kushindwa kupata ushindi na kulazimishwa sare wakiwa nyumbani.
“Hatukucheza kwa kiwango chetu na tatizo ni uchovu waliokuwa nao wachezaji wangu, lakini Watanzania hawapaswi kukata tamaa kwani bado tunayo nafasi ya kurekebisha makosa yetu kwenye mchezo wa marudiano ambao tutacheza kwao Julai 22,”amesema Mayanga.
Kocha huyo amesema wanatambua makosa waliyofanya na watajifua kwa nguvu kuhakikisha wanapindua fikra za Rwanda, ambao walikuja hapa na kucheza kwa kupoteza muda baada ya kufanikiwa kupata bao la mapema.
Amesema atahakikisha anaongea vizuri na wachezaji wake ili kuhakikisha wanacheza kwa kujitoa na kuwabana Rwanda ili waweze kupata bao angalau moja ambalo linaweza kuwapa presha wenyeji wao.
Katika mchezo huo Stars ilitoka sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Rwanda kwenye mechi ya iliyochezwa jana uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages