Hiki hapa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda kitakacho tua jijini Mwanza tare 11 kuiva Taifa stars.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 8 July 2017

Hiki hapa kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda kitakacho tua jijini Mwanza tare 11 kuiva Taifa stars..Timu ya Taifa ya Soka ya Rwanda 'Amavubi' inatarajiwa kuingia Jijini Mwanza ikitokea Jijini Dar es Salaam Julai 11, kwa ajili ya mchezo wa Kuwania fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za Ndani 'CHAN' dhidi ya Tanzania.

Kikosi hicho cha Rwanda kitatua Jijini Dar es Salaam kikitokea Kigali Rwanda na Ndege saa 9 Alfajiri na hapohapo kitaunganisha Kuja Mwanza na Kufikia katika New Mwanza Hotel iliyopo katikati ya Jiji.

Mmoja wa waratibu wa Safari hiyo kwa Upande wa Mwanza Juma Msaka ameuambai Mtandao huu kuwa mipango ya kuwapokea Rwanda imekwishakamilika na Kinachosubiriwa ni wao tu kuingia nchini.

Maandalizi yamekamilika.
-Mipango yote ipo sawa, na tumejaribu kuwatafutia mazingira rafiki ili waweze kufuruhia wakiwa hapa Mwanza, Tumeona tuwachulie vyumba hapa Mwanza Hotel kwani ni karibu na Uwanja wa Nyamagana ambapo watafanya mazoezi" Msaka ambaye pia ni katibu wa chama cha Mpira wilaya ya Ilemela na Msimamizi msaidizi wa Uwanja wa CCM Kirumba Alisema.

Amesema wanatarajia kupokea msafara wa Watu 27 wakiwemo wachezaji 22 kwa ajili ya mchezo huo ambao umepangwa kufanyika Julai 15 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Mchezo huo ni muhimu kwa Kila Timu kwani watarudiana Wiki moja baadae Julai 22, Jijini Kigali Rwanda Hivyo matokeo mazuri katika mchezo huo yataonekana kama Mtaji kuelekea mchezo wa marudiano.


Kikosi Kamili kinachotarajiwa kutua nchini.
Walinda Milango ni  Kwizera Olivier (Bugesera Fc), Ndayishimiye Eric (Rayon Sport) na Nzarora Marcel (Police Fc)
Walinzi Nsabimana Aimable (APR), Imanishimwe Emmanuel (APR), Manzi Thierry (Rayon Sport), Muvandimwe Jean Marie Vianney (Police Fc), Rucogoza Aimable (Bugesera Fc), Bishira Latif (AS Kigali), Kayumba Soter (AS Kigali) and Mpozembizi Mohamed (Police Fc) na Iradukunda Eric (AS Kigali).
Viungo ni Bizimana Djihad (APR), Mukunzi Yannick (APR), Niyonzima Olivier (Rayon Sport), Nshuti Dominique Savio (AS Kigali), Muhire Kevin (Rayon Sport) na Niyonzima Ally (Mukura)
Wakati washambuliaji ni Nshuti Innocent (APR), Mico Justin (Police Fc), Mubumbyi Barnabe (AS Kigali) na Gilbert Mugisha (Pepiniere Fc).

No comments:

Post Bottom Ad

Pages