Hii ndio Sababu ya Vincent Bosou kuondoka Yanga.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 6 July 2017

Hii ndio Sababu ya Vincent Bosou kuondoka Yanga..


Klabu ya Yanga imeshindwa kufikia makubaliano na beki  wake Vincent Bossou ambae kwa sasa ametimkia huko bondeni na kupata katika kikosi cha timu ya Bidvest Wits ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.


Bossou, raia wa Togo, ambaye aliichezea Yanga kwa mafanikio na kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, baada ya kumaliza mkataba Jangwani hivi karibuni, amewachenjia viongozi wa timu hiyo akitaka dau kubwa ambalo wameshindwa kumpa na kuamua kuachana naye.


Kwa mujibu wa barua rasmi tumeinasa inaoneyesha iliandikwa na wakala wake Gibby Kalule kwenda kwa Yanga, beki huyo alitaka dau la usajili la dola 42,000 ambayo ni sawa na Sh milioni 92, mshahara wa dola 4,200 (Sh milioni 9.2) kila mwezi, tiketi mbili za ndege kila mwaka kwa ajili ya yeye na mkewe wakati wa mapumziko pamoja na bonasi ya dola 5,000 (Sh milioni 11) kama timu hiyo itatwaa ubingwa.


Kwa dau hilo, Yanga hawakuwa tayari kulitoa, hivyo kujibu barua kwa wakala huyo kwamba haitawezekana na wanamtakia kila la kheri. Barua hiyo pia tunayo.

Hata hivyo, juzi Jumatatu, Bidvest ilimuandikia barua wakala huyo, ikieleza kuwa imekubali mchezaji huyo awe anafanya mazoezi na timu hiyo, na kama ikivutiwa naye itamsajili au ikiwa vinginevyo atakaa hapo mpaka atakapopata timu huku akihudumiwa kila kitu.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages