Full time Chipolopolo 4 Tanzania 2( stars kusaka mshindi wa 3) - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 5 July 2017

Full time Chipolopolo 4 Tanzania 2( stars kusaka mshindi wa 3)

Timu ya taifa ya Tanzania leo imekubari kipondo cha magoli 4-2 kutoka kwa tiku ya taifa ya Zambia ( Chipolopolo) katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la COSAFA uliopigwa katika uwanja wa Moruleng Stadium   huko nchini Afrika ya kusini.
Katika mchezo huo Stars ilitangulia kupata goli kwa frer kici iliyopigwa na Erasto Nyoni mnamo dakika ya 14' ya mchezo kabla ya vijana wa Chipolopolo kurejesha goli hilo mnamo dakika 44 kupitia kwa Mwila, hata hivyo dakika moja kabla ya kwenda mapumziko Zambia waliongeza bao la pili kupitia kwa Shonga na kuwafanya Zambia kwenda mapumuziko huku wakiwa kifua mbele.

Kipindi chapili zambia walianza kwa kuongezea msumali katika jeneza la Tanzania ambapo dakika ya  56 Chirwa aliiandikia timu yake ya Zambia goli la tatu kwa mkwaju wa penati huku msumali wa mwisho ukipigiliwa na Shonga mnamo dakika ya 68' ,hata hivyo Stars ilijaribu kufurukuta ka kupata goli la pili mnamo dakika ya 84' kupita kwa nyota wake Simon Msuva na hivyo mpaka mwamuzi wa mchezo huo kutoka Afrika ya kusini anaamuru kumalizika kwa mchezo huo Zambia 4-2 Tanzania


Kwa matokeo hayo Tanzania itacheza mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu .

No comments:

Post Bottom Ad

Pages