Chelsea wakubali dili... - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 1 July 2017

Chelsea wakubali dili...


Chelsea wamekubali dili la pauni milioni 33.4 na Roma kumsajili beki Antonio Rudiger, kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky Italia.

Antonio Rudiger, 24 anatarajiwa kufanya vipimo vya afya siku ya  jumatatu na kukamilisha usajili wa mkataba wa miaka mitano.

Sky Italia imearifu kwamba makubaliano ya malipo ya awali ya pauni milioni 29 na baadae ongezeko (add-ons) la pauni milioni 4.4 yamekubalika.

Jana ijumaa sky sports iliarifu kwamba mazungumzo yalikuwa yameanza baina vilabu hivyo viwili kuhusu usajili wa Rudiger ambaye alihamia Roma kutoka Stuttgart majira ya kiangazi yaliyopita kwa dau la pauni milioni 7.6

Na Yego Shola.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages