Yanga wasipozingua hapa wametoboa,kumnasa huyu baada ya Eid. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Sunday, 25 June 2017

Yanga wasipozingua hapa wametoboa,kumnasa huyu baada ya Eid.Beki kisiki wa Mbao FC ya jijini Mwanza, Yusuph Ndikumana, anaweza akamwaga wino kwenye kikosi hicho, ambacho kinafanya kila linalowezekana kujiimarisha kipindi hiki cha usajili.
Taarifa za uhakika kutoka Yanga zinadai kwamba, beki huyo anaweza akatua muda wowote baada ya kumalizika kwa Sikukuu ya Eid el Fitri, hiyo ikimaanisha kuwa, watakuwa wamewazidi ujanja mahasimu wao, Simba, ambao walikuwa wakimfukuzia.
“Unajua yule jamaa (Ndikumana) ni moja ya mabeki imara sana, kwani kila mmoja aliona shughuli yake msimu uliokwisha, kutokana na kazi yake hiyo tumekuwa tukimmezea mate na haitashangaza baada ya kumalizika kwa sikukuu hiyo iliyopo mbele yetu (Eid el Fitri), tukamalizana naye.
“Tunataka kuimarisha kikosi chetu, kwani kama unavyojua mwakani tutashiriki kwa mara nyingine michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo mara hii tumeamua kufika mbali, tofauti na misimu iliyopita, pia tukitaka kutwaa tena ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya nne mfululizo,” alisema.

Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages