WENGER ATAMBA USAJILI WA KOLASINAC - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 8 June 2017

WENGER ATAMBA USAJILI WA KOLASINAC

 Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuidaka saini ya mchezaji Sead Kolasinac.
Mchezaji huyo mwenye miaka 23 ameangukia mikononi mwa Wenger ambaye anajipanga kukisuka kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.
Wenger alisema mchezaji huyo ni muhimu kwa maendeleo ya klabu hiyo na anaamini ataisaidia kwa kiasi kikubwa.
Mchezaji huyo alijiunga na timu  ya vijana ya Schalke mwaka 2011 kabla ya kutinga timu ya wakubwa kwenye Bundersliga mwaka 2012 na kucheza jumla ya mechi 123 klabuni hapo.
Mchezaji huyo raia wa Bosnia-Herzegovina atarajiwa kuvuta Pauni 7.5 wakati wa mkataba wake atakapokuwa na Arsenal.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages