WAGENI WENGINE WA LIGI KUU TANZANIA BARA WAANZA KUNYOFOA NYOTA KUTOKA LIGI KUU.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 19 June 2017

WAGENI WENGINE WA LIGI KUU TANZANIA BARA WAANZA KUNYOFOA NYOTA KUTOKA LIGI KUU..


Kiungo African Lyon, Awadh Juma yupo mbioni kujiunga na Njombe Mji iliyopanda daraja msimu huu.

Njombe Mji iliyopania kufanya vizuri ikiwa chini ya makocha Hassan Banyai na Mrage Kabange wanasaka wachezaji wenye uzoefu wa kumalisha kikosi chao.

Awadh alikuwa na msimu mzuri katika timu ya Lyon, lakini alishindwa kuisaidia timu hiyo kuepuka janga la shuka daraja.

Kiungo huyo alisema bado tupo katika mazungumzo na viongozi wa Njombe kuangalia uwezekano wa kujiunga nao.

“Nilifanya mazungumzo na viongozi wa Njombe wakionyesha kuwa wanataka niende kule mimi sina hiyana niliwapa namba ya meneja wangu, uzuri kwamba meneja amenambia wapo sehemu nzuri ya maongezi kwahiyo muda wowote natua Njombe,” alisema Awadh.


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages