Usajili Yanga wafuatao kutemwa na hawa kusalia kikosini.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 30 June 2017

Usajili Yanga wafuatao kutemwa na hawa kusalia kikosini..


Baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu  2016-17 kumalizika baadhi ya vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo vimekua vikifanya maandalizi kwa kufanya usajili huku vilabu vingine vikiwatema baadhi ya wachazaji.

Klabu ya Yanga ni moja ya klabu zinazo shiriki ligi hiyo n huu ndio uamziki wake na maandalizi ya msimu ujao.


Mazungumzo kati ya Yanga na beki wake kisiki, Vincent Bossou yanaonekana kukwama na tayari viongozi wa klabu hio wameinua mikono. Bossou alijiunga Yanga mwaka 2015 akitokea ligi daraja la pili Korea Kusini.

Mshambuliaji Malimi Francis Busungu ameoneshwa mlango wa kutokea baada ya kumaliza msimu kwa kucheza mechi moja tu ya ligi ambayo hata hivyo alipumzishwa baada ya dakika 32 tu za kipindi cha kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kiungo mkabaji, Justine Zulu anaripotiwa kuwa mbioni kutemwa na Yanga. Zulu alisajiliwa wakati wa dirisha dogo lakini baada ya kucheza mechi 8 tu za Ligi anaonekana kutokuwa na msaada mkubwa katika kikosi cha kwanza.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe naye ameongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga akifuata nyayo za Donald Ngoma.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga licha ya awali kuhusishwa na kusaini mkataba na klabu ya Polokwane City ya Afrika Kusini.


Donald Ngoma akiandika nakala ya mkataba wake

Beki Gadiel Michael Mbaga wa Azam anaripotiwa kumalizana na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.

Wakati Gadiel akiwa mbioni kutua Yanga, Mwinyi Haji amemaliza mkataba wake na haijulikani kama ataongezewa mkataba mpya.Beki Abdallah Hajji ‘ Ninja’  kutoka Taifa Jang’ombe alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Yanga mwanzoni mwa mwezi wa Juni.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages