USAJILI YANGA: MSUVA AGOMA KUNG'OKA JANGWANI.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 14 June 2017

USAJILI YANGA: MSUVA AGOMA KUNG'OKA JANGWANI..


Baada ya kuwako na taarifa za nyota wa klabu ya Yanga Simon Msuva kutajwa kutimkia klabu ya Zamaleck, taarifa zinasema kua amekataa kuondoka klabuni humo.
Msuva, amesema bado ana mkataba na kikosi cha timu yake hiyo na ataendelea kukitumikia kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Msuva ni miongoni mwa wachezaji ambao wanahusishwa kwenda kwa wekundu wa Msimbazi, Simba, ambao wamedaiwa kutaka kumng’oa mchezaji huyo ndani ya viunga vya Jangwani kwa lengo la kuimarisha kikosi chao.
“Ofa nyingi zimekuja, lakini mimi bado nina mkataba na Yanga, lakini suala hilo nauachia uongozi na  meneja wangu kama Mungu atakuwa amepanga niondoke nitaondoka, kama itakuwa bado basi nitaendelea kuwapo,” alisema.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages