USAJILI: WAZIRI JUNIOR ATUA AZAM FC : - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 5 June 2017

USAJILI: WAZIRI JUNIOR ATUA AZAM FC :Mshambuliaji wa Toto Africa aliyekuwa akiwindwa na klabu ya  Yanga  amekamilisha taratibu zote na kutia saina mkataba wa kuitumika klabu ya Azam FC kwa kandarasi ya miaka miwili mkataba utakao mfanya kurndelea kusalia katika klabu hiyo hadi mwaka 2019.

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kuwataarifu mashabiki wa soka nchini kuwa leo umefanikiwa kuingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji anayekuja kwa kasi hivi sasa nchini, Wazir Junior.

Junior aliyependekezwa na Kocha Mkuu Aristica Cioaba, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao 2017-18, ambapo alikuwa straika kinara wa Toto African ya Mwanza msimu uliopita, akiwa mfungaji wao bora kwa mabao sita aliyofunga.

Zoezi la kuingia mkataba kwa pande hizo mbili limefanyika leo mchana kwenye Ofisi za Mzizima, zilizopo barabara ya Nyerere, Dar es Salaam, na kusimamiwa na Meneja Mkuu wa Azam FC, Abdul Mohamed, aliyekuwa sambamba na viongozi wengine Meneja wa timu, Phillip Alando na Ofisa Habari, Jaffar Idd.

kwa Habari Kamili Tembelea :www.azamfc.co.tz

No comments:

Post Bottom Ad

Pages