USAJILI WA BUSWITA YANGA YAPATA KIBURI.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 17 June 2017

USAJILI WA BUSWITA YANGA YAPATA KIBURI..Katika muendelezo zile tambo za miongoni mwa klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania hasa katika kipindi hiki cha usajili.


Klabu ya Yanga imewapiku wapinzani wao Simba kwa kufanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa Mbao FC, Pius Buswita.
Yanga imempa mkataba wa miaka miwili mshambuliaji huyo, baada ya kufikia makubaliano ikiwa ni siku mbili baada ya viongozi wa Simba kutamba kuwa wamemsajili mchezaji huyo.


Mjumbe wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Yanga Husseni Nyika, ameiambia Goal, wameanza kuzima midomo ya wapinzani wao ambao walisema hawana fedha za usajili kwa kumyakua mchezaji huyo.
“Yanga tupo vizuri na kazi zetu tumeamua kufanya kimya kimya kwa sababu tunazo hela za kutosha zinazotuwezesha kufanya usajili tunaoutaka kwa hiyo wanaosema hatuna fedha wajiandae wasishangae tukivunja ngome zao,” amesema Nyika.


Kiongozi huyo amesema wanachofanya hivisasa ni kutimiza maneno yao ya kumsajili mchezaji yeyote wanayemtaka kutokana na ukubwa wa mashinda yanayowakabili msimu ujao.
Nyika amesema wanataka kutetea ubingwa wao lakini pia kufika mbali kwenye michuano ya kimataifa hilo linawezekana kutokana na mipango mkakati waliyokuwa nayo tangu msimu haujamalizika.
Buswita anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa mpya baada Abdallah Haji ‘Ninja’ na Gadiel Michael wa Azam FC.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages