USAJILI TUNAOFANYA SIO WA KUMKOMOA MTU, NA WANAOSEMA HIVYO NI WAZUSHI TU. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Thursday, 22 June 2017

USAJILI TUNAOFANYA SIO WA KUMKOMOA MTU, NA WANAOSEMA HIVYO NI WAZUSHI TU.


Makamu wa Rais wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu, amesema kamati ya Usajili inafanyakazi kutokana na ripoti ya Mwalimu Joseph Omog, na Si kwa hulka zao wenyewe na kila anayesajiliwa ana baraka kutoka katika Benchi la Ufundi la Timu yao. 
 -Mwalimu ameacha ripoti yake ambayo sisi tunaifahamu na Ndio tunayotumia kwa Usajili, sasa huyo anayesema pembeni kwamba Simba inasaini kwa maelekezo ya Nje ya ripoti ya Omog sasa aje atuambie kama anayo hiyo ripoti" Amesema. 

Kaburu amewaita wale Wote wanaosambaza taarifa Ya kwamba wanafanya Usajili wa kuwakomoa wengine ni wazushi ambao Hawajui lolote kuhusu klabu yao. 
-Haya ni Maneno ya kuzusha tu tena na watu ambao hawaujui Mpira kwa sidhani kama Nina muda wa kuanza kubishana nao, Ila tu kwa kifupi uongozi Upo makini na Unajua unataka nini lengo ni kupata timu bora msimu ujao" Kaburu aliongeza.


Download app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages