TETESI ZOTE ZA USAJILI ULAYA LEO JUNE 21. 2017 - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 21 June 2017

TETESI ZOTE ZA USAJILI ULAYA LEO JUNE 21. 2017


CHELSEA YAPANGA KUMSAJILI LEWANDOWSKI
Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji matata wa Bayern Munich Robert Lewandowski, kwa mujibu wa habari kutoka  Mirror . 

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Poland amefunga mabao 30 kwenye Ligi ya Bundesliga msimu uliopita lakini hana furaha na maisha ya Allianz Arena.

Kocha wa Blues yupo tayari kutumia fursa ya mchezaji huyo kutokuwa na raha klabuni kwake kumsajili kuziba pengo la Diego Costa.

MAN UTD WANAMTAKA LUKAKU WA £90M
Manchester United hawajakata tamaa katika jitihada zao kumsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku, Lakini watalazimika kulipa paundi milioni 90 limeripoti  the Mirror.  

Inaaminika Mbelgiji huyo amekubali dili kutua Chelsea, ingawa United na mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich bado wanaweza kuinasa saini yake.

ARSENAL KUMPA RAMSEY MKATABA MPYA
Arsenal wameanza mazungumzo ya mkataba mpya na kiungo wao mahiri Aaron Ramsey, kwa mujibu wa habari za  the Telegraph.  

Alexis Sanchez, Mesut Ozil na Alex Oxlade-Chamberlain hawana uhakika wa kubaki klabuni hapo jambo linalomsukuma Arsene Wenger kufanya jitihada za kuwabakisha wachezaji wake wengine klabuni hapo..

SALAH ACHAGUA JEZI YAKE LIVERPOOL
Mchezaji mpya wa Liverpool Mohamed Salah anataka kuwa nambari tisa mpya, kwa mujibu wa habari kutoka Liverpool Echo .

Uhamisho utakaomleta Mmisri huyo Anfield unatarajiwa kutangazwa ndani ya wiki kwa dili la kuvunja rekodi ya klabu kwa zaidi ya paundi milioni 35.

Na Salah, ambaye alivaa jezi nambari 11 Roma, yupo tayari kuvaa namba 9 ambayo iliachwa wazi na Christian Benteke aliyehamia Crystal Palace mwaka jana.

BARCA KUFANYA USAJILI WA REKODI KWA DEMBELE
Barcelona wanataka kufanya uhamisho wa kuvunja rekodi kwa kumsajili nyota wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, kwa mujibu wa  Bild .

Mkurugenzi wa michez Robert Fernandez ni shabiki mkubwa wa mshambuliaji huyo wa BVB mwenye mkataba hadi 2021. Uhamisho huo utakuwa mauzo makubwa katika historia ya Bundesliga kwani utazidi euro milioni 75 Manchester City walizolipa kwa ajili ya Kevin De Bruyne 2015.

JUVENTUS YAMWANIA NEVES
Juventus imeungana na Liverpool na Chelsea katika mbio za kumfukuzia nyota wa Porto Ruben Neves, Mirror limeripoti.

MAN UTD HUENDA ISIMSAJILI RONALDO
Manchester United wanasita-sita kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid, kwa mujibu wa  Daily Express .

Ronaldo inaaminika anatamani kuondoka Real Madrid, lakini Jose Mourinho anaogopa kuingia kwenye mbio hizo za kumsajili. United wanahofu ni hila za Ronaldo tu kutaka kupewa dili nono zaidi Madrid na hawataki kutumia muda kufanya mazungumzo na mchezaji ambaye hawatamsajili.

MAN CITY HAWANA MPANGO NA AUBAMEYANG
Manchester City hawajaandaa dau la paundi milioni 60 kwa ajili ya Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang kama tetesi zinavyodai, limeripoti  BBC .

OXLADE-CHAMBERLAIN KWENYE RADA UINGEREZA
Kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain yupo kwenye rada za Chelsea, Liverpool na Manchester City msimu wa majira ya joto, kwa mujibu wa Sky Sports.  

PEPE AMTAKA RONALDO KUTUA PSG
Pepe amemtaka Cristiano Ronaldo kuungana naye PSG baada ya mshambuliaji huyo kuonyesha nia ya kutaka kuondoka Real Madrid, kwa mujibu wa  El Transistor .

MAN UTD INATAKA KUMSAJILI SEMEDO
Manchester United wanaandaa upya ofa wakitaka kumsajili mchezaji wa Benfica Nelson Semedo baada ya kumsajili Victor Lindelof ambaye waliwahi kuwa kwenye timu moja, kwa mujibu wa  O Jogo .

LYON WATARAJIA KUMSAJILI TRAORE
Lyon ni miongoni mwa timu zinazopambana kukamilisha dili la paundi milioni 16.6 kumsajili Bertrand Traore kutoka Chelsea, kwa mujibu wa Evening Standard .

MATHIEU AKARIBIA KUTUA SPORTING
Beki wa Barcelona Jeremy Mathieu amesafiri hadi Ureno kukamililisha uhamisho kujiunga na Sporting Lisbon, kwa mujibu wa  A Bola .

BAYERN YAMFUKUZIA WALKER
Bayern Munich inataka kumsajili Kylie Walker kutoka Tottenham Hotspur, kwa mujibu wa  T he Sun .

Ada ya Muingereza huyo inakadiriwa kuwa paundi milioni 45.

ASANO AKATALIWA KUREJEA ARSENAL
Takuma Asano atabaki kwa mkopo Stuttgard akitokea Arsenal kwa msimu mmoja zaidi, limeripoti jarida za Ujerumani  Bild . 

ARSENAL IPO TAYARI KUTOA €30M KUMSAJILI TURAN
Arsenal wanaandaa dau la euro milioni 30 kumsajili Arda Turan kutoka Barcelona, kwa mujibu wa ripoti kutoka  Uturuki na Spain .

MBAPPE AMEICHAGUA MADRID
Kylian Mbappe ameiweka wazi Monaco kuwa anataka kujiunga na Real Madrid majira ya joto, limeripoti jarida la  Marca .

JUVE & ARSENAL ZAMWANIA ASENSIO
Marco Asensio anafikiria kuondoka Real Madrid uhamisho wa majira ya joto, Juventus na Arsenal zinavutiwa na huduma yake, limeripoti Diario Gol .

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 alijiunga na Madrid akitokea Mallorca miaka mitatu iliyopita na ameonyesha mwanga wa kufanikiwa, lakini anataka muda zaidi wa kucheza. 

BVB WANAMTAKA NYOTA HUYO WA BARCA
Borussia Dortmund wanajipanga kumsajili mchezaji wa Barcelona Lee Seung-Woo, Bild  limesema.

UTD & BAYERN ZAMFUATILIA DEMBELE
Manchester United na Bayern Munich watamfuatilia kinda wa Celtic mwenye umri wa miaka 14 Karamoko Dembele katika shindano la vijana majira ya joto, The Sun  limeripot i.
Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages