TETESI ZOTE ZA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA WIKI HII.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 17 June 2017

TETESI ZOTE ZA USAJILI LIGI KUU TANZANIA BARA WIKI HII..EMMANUEL OKWI MBIONI KUTUA SIMBA

Wakati mshambuliaji Ibrahim Ajib akiwa anaelekea Jangwani, klabu ya Simba inaonekana kutokuwa na shida juu ya hilo kwasababu tayari ipo njiani kumvalisha Emannuel Okwi Jezi nambari 25 msimu ujao.

“Ni kweli nipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Simba, naamini tutakubaliana kila jambo na nitasaini kuichezea tena Simba.” – alisema Okwi.

KAGERA SUGAR YATAKA MIL 150 USAJILI WA MBARAKA YUSUF

Kegera Sugar hawaelewi lolote kuhusiana na mshambuliaji Mbaraka Yusuf, wanasema ni mali yao, kwa mujibu wa Championi .

Msisitizo wa Kegera Sugar wanasema wanataka walipwe shilingi milioni 150 ili imuachie mshambuliaji huyo kwenda Azam FC ambako tayari amesaini.

Hatua hiyo imekuja siku chache tangu Meneja wa Kagera, Mohammed Hussein kupiga hodi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akidai mshambuliaji huyo amesajiliwa kimakosa.

BOSSOU KUTUA SINGIDA AU ULAYA

Beki wa Yanga, Vincent Bossou kwa sasa ana ofa nne mkononi lakini mwenyewe ameibuka na kusema kuwa tatu kati ya hizo ndizo amezipa kipaumbele, kwa mujibu wa Shaffihdauda .

Bossou ambaye amekwenda Dubai kwa mapumziko ya Siku 10, amethibitisha kupokea ofa nne kutoka Singida United ya Tanzania na timu 3 za Ulaya.

“Nimepata ofa nchi tatu, kama mambo yataenda vizuri nikitoka Dubai nitaunganisha kwenda Uturuki kufanya mazungumzo ila kwa sasa siwezi kukutajia kwa sababu bado mapema sana,” alisema Bossou.

“Kwa Tanzania nimepata ofa Singida United, wenyewe wako tayari kunipa fedha nzuri, ikiwemo dau la usajili na mshahara mnono, hivyo mambo yakiwa magumu nitarudi kuwasikiliza.”

SINGIDA UNITED YAMNASA DEUS KASEKE

Deus Kaseke ni kati ya wachezaji 13 waliopo kwenye orodha ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika mwishoni mwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Uongozi wa Singida United umemuandalia mkataba kiungo mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke kwa ajili ya kuusaini huku wakimwambia apumzike kwanza kabla ya kuusaini.

JONAS MKUDE AKUBALI KUTUA YANGA

Jonas Mkude kwa sasa yuko huru kujiunga na timu yoyote baada ya mkataba wake na Simba kudaiwa kumalizika hivi karibuni, ikiwa ni mwisho wa mkataba wake wa shilingi milioni 60 aliosaini kuitumikia Simba miaka miwili iliyopita.

Kiungo huyo amesema atakuwa tayari kusaini mkataba na Klabu ya Yanga kwa dau la kuanzia milioni 70 kwenda juu kutokana na kiwango alichonacho kwa sasa, kwa mujibu wa gazeti la Championi.

AZAM YAMNASA WAZIRI JUNIOR KUTOKA TOTO

Klabu ya Azam FC imemnasa mshambuliaji anayekuja kwa kasi hivi sasa nchini, Wazir Junior.

Junior aliyependekezwa na Kocha Mkuu Aristica Cioaba, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao 2017-18, ambapo alikuwa straika kinara wa Toto African ya Mwanza msimu uliopita, akiwa mfungaji wao bora kwa mabao sita aliyofunga.

AZAM KUZUNGUMZA NA MANULA NA KAPOMBE

Azam FC imesema kwamba ipo kwenye mazungumzo na wachezaji wake wawili wanaohusishwa na mpango wa kutaka kuhamia Simba, kipa Aishi Manula na beki, Shomary Kapombe.

Wawili hao wote wanamaliza mikataba yao mwezi huu na imekuwa ikiripotiwa kwamba wako kwenye mipango ya kujiunga na Simba SC. Msemaji wa Azam, Jaffar Iddi amesema mazungumzo yanaendelea na watasaini mkataba mpya.

SIMON MSUVA SAFARI IMEFIKA KUONDOKA YANGA

Timu tatu kutoka katika nchi tatu, sasa zinataka kumsajili winga mahiri wa Yanga, Simon Msuva. Timu hizo zinatokea katika nchi za Morocco, Misri na Afrika Kusini na Msuva amethibitisha hilo.

Kulingana na Saleh Jembe, Simon Msuva amedai kuwa ofa hizi ni kweli zimetua kwenye meza ya Yanga naye ana taarifa kamili kuhusu kila kinachoendelea.

AJIBU NA MKUDE RUKSA KUONDOKA SIMBA

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema timu yake imechoshwa na kauli zisizoeleweka za wachezaji Jonas Mkude, Abdi Banda na Ibrahim Ajibu kuhusu usajili mpya, hivyo kamaa wanataka kuondoka ruksa, GLOBAL TV online iliripoti.

Mikataba ya wachezaji hao tayari imemalizika mwishoni mwa msimu uliopita na sasa wanatajwa kuondoka kwenda kwenye moja za klabu za hapa nchini.

DONALD NGOMA NA NIYONZIMA KUTUA SIMBA

Taarifa kutoka ndani ya Simba zimedai kuwa Donald Ngoma na Haruna Niyonzima wa Yanga wanakaribia kumwaga wino wa miaka miwili kutua Msimbazi, kwa mujibu wa Shaffihdauda .

Simba imekuwa ikiwawania Ngoma na Niyonzima tangu msimu uliopita ambapo sasa imeonekana kukaribia kuwanasa wote wawili kutokana na mikataba yao kufikia ukingoni. Ingawa italazimika kupunguza baadhi ya wachezaji wake wa kigeni kutimiza idadi ya wachezaji saba.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages