TETESI ZA USAJILI ULAYA LEO JUNE 23. 2017.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 23 June 2017

TETESI ZA USAJILI ULAYA LEO JUNE 23. 2017..


FABINHO THAMANI YAKE €45M
Kiungo wa Monaco Fabinho anapatikana kwa ada ya uhamisho isiyopungua euro 45 millioni, kwa mujibu wa  Calcio Mercato .

Juventus, Manchester United, Manchester City na Paris Saint-Germain zinataka kumsajili Mbrazili huyo mwenye umri wa miaka 23..

ZIDANE AZUNGUMZA NA MBAPPE
Zinedine Zidane ameshazungumza na Kylian Mbappe katika harakati zake za awali kumshawishi Mfaransa huyo kutua Real Madrid, kwa mujibu wa  L'Equipe .

Goal  inafahamu kwamba PSG wametoa ofa ya €135 million i kwa ajili ya mchezaji huyo mahiri wa Monaco lakini Real Madrid wapo kwenye nafasi nzuri zaidi kumsajili kwani Florentino Perez anahitaji saini yake.

MAN UTD YAMTAKA ALBA
Manchester United wamelenga kumsajili mchezaji mahiri wa Barcelona Jordi Alba, kwa mujibu wa  ESPN .

Jose Mourinho anatafuta beki wa kushoto majira ya joto, lakini usajili wa Alba si rahisi sana kwani mchezaji huyo ametulia vizuri Camp Nou.

SPURS YAVUTIWA NA SUSO
Tottenham wanavutiwa kumsajili kiungo wa AC Milan Suso, Kwa mujibu wa  Marca .

Milan bado hawajamfunga kinda huyo wa zamani wa Liverpool kwa mkataba mpya San Siro,  na Mauricio Pochettino anataka kuhakikisha mchezaji huyo anatua London katika jitihada za kuunda kikosi thabiti cha ushindani Ligi ya Mabingwa.

DE BOER APEWA KIBARUA CHA PALACE
Frank de Boer amepewa fursa ya kumrithi Sam Allardyce kama meneja mpya Crystal Palace  Guardian limeripoti.

De Boer amewahi kuinoa Ajax lakini hakupata mafanikio yoyte zaidi ya timu hiyo kudidimia kabisa.

ARSENAL YAMLENGA BUTLAND
Arsenal wamemfanya Jack Butland wa Stoke City chaguo nambari moja usajili wa mlinda mlango kurithi nafasi ya Petr Cech, kwa mujibu wa Bleacher Report .

Baada ya kumkosa Jorda Pickford aliyejiunga na Everton, Washika Mtutu hao wa London wamehamishia majeshi kwa Muingereza Butland kujiandaa na maisha bila ya Cech.

OFA YA MAN UTD KWA GOMES YAKATALIWA
Ofa ya Manchester United ya paundi milioni 31 kwa ajili ya kiungo wa Barcelona Andre Gomes imekataliwa, kwa mujibu wa  Catalunya Radio  via  The Sun .

LIVERPOOL YAKATAA KUMUUZA MORENO
Liverpool wamekataa ofa ya paundi milioni 11 kutoka Napoli kwa ajili ya beki Alberto Moreno, kwa mujibu wa  The Times .

Ingawa Reds wapo tayari kumuuza mchezaji huyo majira ya joto, hawapo tayari kumwachia kwa kiasi chochote chini ya £15m.

JAMES ANAPENDELEA KUTUA MAN UTD
James Rodriguez amepokea ofa kutoka Manchester United na Chelsea, chanzo cha OK Diario kikidai kuwa mchezaji huyo anapendelea kwenda Man United.

COURTOIS BADO HAKIELEWEKI
Thibaut Courtois bado anaitoa jasho Chelsea kuhusu mustakabali wake baada ya kukataa kusaini mkataba mpya, limeripoti The Sun .

ZIDANE ANAMTAKA BONUCCI
Bosi wa Real Madrid Zinedine Zidane anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki wa kati wa Juventus Leonardo Bonucci, kimedai  Diario Gol .

FOXES WAMTOLEA MACHO IHEANACHO
Leicester City imeonesha nia ya kumsajili mchezaji wa Manchester City Kelechi Iheanacho, kwa mujibu wa  The Sun .


Down load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages