TETESI ZA USAJILI ULAYA LEO JUNE 12..2017 - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 12 June 2017

TETESI ZA USAJILI ULAYA LEO JUNE 12..2017CITY KUMFANYA ALEXIS KUWA KIBOPA


Manchester City wamejipanga kumsajili Alexis Sanchez kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo, limeripoti  Daily Star .

Pep Guardiola anataka kuimarisha safu yake ya ushambulizi na yupo tayari kumlipa kiungo huyo paundi 275,000 kwa wiki.

ZLATAN ANAWEZA KUBAKI UNITED


Zlatan Ibrahimovic anaweza kupewa mkataba mwingine kubaki Manchester United, kwa mujibu wa  Manchester Evening News .

BARCA KUMLIPIA €80M VERRATTI


Marco Verratti ameomba kuondoka Paris Saint-Germain, baada ya kumwambia mkurugenzi wake mpya Antero Henrique kwamba hana raha kubaki tena Parc des Princes, L'Equipe  limeripoti.

Barcelona na Bayern Munich, ambako Carlo Ancelotti ni shabiki mkubwa wa Muitaliano huyo zipo tayari kutoa euro milioni 80 kuipata saini yake.

MORATA AMTAKA BALE KUUNGANA NAYE MAN UTD


Alvaro Morata amemtaka Gareth Bale ahame Real Madrid ili watue wote Manchester United, kwa mujibu wa  Don Balon .

Goal inafahamu kwa  Morata yupo kwenye rada za United na AC Milan inaongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji huyo wa Real Madrid .

MAHREZ AISUBIRI BARCELONA


Winga wa Leicester City Riyad Mahrez anaisubiria Barcelona itoe dau kumsajili anapojipanga kuachana na mbingwa wa Ligi Kuu Uingereza wa 2016, kwa mujibu wa  Sport .

Mahrez ameripotiwa kupokea ofa kutoka Arsenal na Chelsea lakini angependelea kujiunga na Barca kucheza La Liga.

ARSENAL YAMFUKUZIA CALHANOGLU


Arsenal wamepania kuizidi ujanja Chelsea kumsajili kiungo aw Bayer Leverkusen Hakan Calhanoglu, kwa mujibu wa  Aksam .

Chelsea walikuwa wakivutiwa muda mrefu na Calhanoglu, lakini kwa sasa Arsenal na Lazio zinakaribia kumnasa kwa dau la €20 millioni. 

ZLATAN MBIONI KUTIMKIA GALAXY


Zlatan Ibrahimovic amekubali kujiunga na Los Angeles Galaxy baada ya kuachiliwa na Manchester United, kwa mujibu wa  Marca .

MAN UTD YAPATA CHANGAMOTO KUMSAJILI KEANE


Manchester United inakabiliwa na ushindani kumsajili beki wa Burnley Michael Keane, kwa mujibu wa  Sky Sports .

Jose Mourinho anataka kumrejesha Keane Old Trafford lakini Ronaldo Koeman naye anatamani kumsajili beki huyo.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages