TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUNE 13 2017.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 13 June 2017

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUNE 13 2017..Chelsea wanajiandaa kumsajili mshambuliaji wa Napoli, Lorenzo Insigne wanapojiandaa kwa maisha bila ya Eden Hazard, kwa mujibu wa The Sun .

Real Madrid wapo mbioni kutoa dau nono kwa ajili ya Hazard, na Antonio Conte anataka kupata mbadala wake haraka kuepuka usumbufu majira ya joto.

BARKLEY HURU KUONDOKA EVERTON

Everton wapo tayari kumruhusu Ross Barkley kuondoka klabuni hapo majira ya joto baada ya kukataa fursa ya kuwa mchezaji anayepokea mshahara mkubwa zaidi katika klabu hiyo, kwa mujibu wa   Mirror .

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekataa dili la £100,000 kwa wiki katika Goodison Park, na sasa Ronaldo Koeman anataka kusajli wachezaji wawili kuziba pengo lake.

GRIEZMANN AONGEZA MKATABA ATLETICO

Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann amesaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Hispania hadi 2022, kwa mujibu wa Marca .

Mustakabali wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa ulikuwa gumzo katika tetesi za vichwa vya habari akihusishwa na tetesi za kutua Manchester United.

RENATO AITOSA MAN UTD

Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches ataitosa Manchester United ili aweze kujiunga na Barcelona, kwa mujibu wa Daily Mail .

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno, 19, aling'ara katika michuano iliyopita ya Euro 2016 na akajiunga na Bayern Munichi aktokea Benfica.

Hata hivyo Sanches atauzwa baada ya kushindwa kuonyesha kandanda safi Bundesliga kwenye kikosi cha Bayern Munich. 

LIVERPOOL YAWASILIANA NA MBAPPE

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amewasiliana na mawakala wa Kylian Mbappe, Wekundu hao wa Anfield wakimtengea Mfaransa huyo paundi milioni 100 kwa mujibu wa  the Daily Mail .

Real Madrid wanaaminika kuwa mstari wa mbele kumwania mchezaji huyo sambamba na Arsenal, Manchester City na Manchester United.

LIVERPOOL YAKARIBIA KUMSAJLI SALAH KWA £35M

Liverpool wanakaribia kufikia makubaliano kumsajili winga wa Roma, Mohamed Salah, kwa mujibi wa Corriere dello Sport .

Kiasi cha awali cha paundi milioni 35 kinatarajiwa kutolewa , na paundi milioni 4 zitaongezwa baadaye, mchezaji huyo ni kipaumbele cha kwanza majira ya joto kwa Jurgen Klopp.

CHELSEA YAONGOZA MBIO ZA JAMES

Chelsea wapo mbele ya Manchester United na Inter Milan katika mbio za kumfukuzia kiungo wa Real Madrid James Rodriguez, kwa mujibu wa  AS.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia anataka kuondoka Real Madrid na anayo machaguzi mengi katika klabu za Ulaya.

CITY KUMFANYA ALEXIS KUWA KIBOPA

Manchester City wamejipanga kumsajili Alexis Sanchez kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo, limeripoti  Daily Star .

Pep Guardiola anataka kuimarisha safu yake ya ushambulizi na yupo tayari kumlipa kiungo huyo paundi 275,000 kwa wiki.

ZLATAN ANAWEZA KUBAKI UNITED


Zlatan Ibrahimovic anaweza kupewa mkataba mwingine kubaki Manchester United, kwa mujibu wa  Manchester Evening News.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages