TANZANIA PRISONS YAMTUPILIA MBALI BANDA YAWANASA HAWA WANNE. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 6 June 2017

TANZANIA PRISONS YAMTUPILIA MBALI BANDA YAWANASA HAWA WANNE.


Klabu ya Tanzania Prisons imepanga kusajili wachezaji wanne wapya huku ikimtema mchezaji mmoja kati ya kikosi chake cha sasa.
Mmoja wa viongozi wa klabu hiyo amesema mchezaji anayeachwa ni George Banda na usajili wa wachezaji wapya utakuwa ni wachezaji wanne.
Meneja wa Prisons, Enock Mwanguku alisema baada ya kupokea ripoti ya kocha Abdallah Mohamed wanatarajia kukaa kikao kesho au keshokutwa  kwa ajili ya kujadili ripoti hiyo.
 “Tutasajili nafasi nne, lakini hadi sasa hatujaanza mikakati yetu na siwezi kusema ni nani tumeanza naye mazungumzo,”alisema Mwanguku.
Alisema “Wachezaji wengine wote tutaendelea nao kwa msimu ujao kutokana na kuonyesha kiwango na kuipigania timu yetu, kwa hiyo Prisons ya msimu uliopita itabadilika kidogo,’’alisema
Kuhusu kuachwa kwa Banda, Mwanguku alisema kuna asilimia kubwa za kuachana na mchezaji huyo kutokana na kutoonyesha kuisaidia timu hiyo.
Alisema sababu ya kuachwa kwake ni kwamba hata alipokuwa akipewa nafasi ya kucheza uwanjani alikuwa haonyeshi kiwango kizuri kama ilivyokuwa kwa wachezaji wenzake.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages