TAIFA STARS YABANWA MBAVU NA LESOTHO IKIWA NYUMBANI - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 10 June 2017

TAIFA STARS YABANWA MBAVU NA LESOTHO IKIWA NYUMBANITimu ya taifa ya Tanzani imelazimishwa sare ya goli moja kwa moja dhidi ya taifa ya Lesotho katika mchezo wa kufuzu kucheza mashindano ya AFCON.

Katika mchezo huo Stars ilotangulia kupata bao mnamo dakika ya 27' kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa anaekipiga katika klabu ya KRC Genk ya nchini Uberigiji kabla ya dakika ya 34' mchezaji Thapelo kutoka Lesotho kuisawazishia timu yake na kufanya ubao kusomeka goli 1-1 magoli yaliyodumu hadi kutamatika kwa kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili kilanza kwa utulivu wa hali ya juu na umakini licha ya kuonekana baadhi ya makosa katika kipindi hicho na makocha kufanya mabadiliko lakini hayakuzaa matunda kwani timu hizo zimetoshana nguvu tena na kuimaliza ngwe hii ya pili pasi na kufungana hivyo ushindi uliopatikana kipindi cha kwanza ukaendelea kutawala.

Hadi Mwamuzi anapuliza kipenga cha kuashiria kumalizika kwa mchezo huo Taifa stars 1 -  1 Lesotho.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages