TAARIFA KWA UMMA kutoka klabu ya Simba.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Friday, 30 June 2017

TAARIFA KWA UMMA kutoka klabu ya Simba..


TAARIFA KWA UMMA Klabu ya Simba kwa masikitiko makubwa inaungana na Wanachama na Washabiki wake katika kipindi hiki kigumu, ambacho viongozi wetu wakuu wa Klabu wapo mahabusu kwa tuhuma kadhaa zilizopo ktk Mahakama ya Kisutu. Viongozi hao Rais Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange Kaburu wamekosa dhamana kwa kuwa mashtaka yao hayadhaminiki kwa mujibu wa sheria za nchi. Klabu kwa sasa imeandaa jopo la mawakili litakalowatetea viongozi wetu hao na linaamini Mahakama itatenda haki kwa pande zote zinazohusika na Shauri hilo. Kesho Jumamosi kamati ya Utendaji ya klabu itakutana pamoja na mambo mengine kuangalia masuala mengine muhimu ya klabu yasikwame,wakati huu ambapo viongozi wetu wapo mahabusu. Tunaamini kamati ya utendaji itakuja na majawabu sahihi ya kuhakikisha shughuli za klabu zinaendelea kama kawaida. Tunawaomba wanachama na washabiki wetu mtulie na tutawapa taarifa rasmi mara baada ya kikao cha kesho Imetolewa na.. Idara ya Habar na mawasiliano Simba Sc.

A post shared by Haji S Manara (@hajismanara) on

No comments:

Post Bottom Ad

Pages