Suleiman Matola kibaruani Lipuli FC - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 28 June 2017

Suleiman Matola kibaruani Lipuli FC

Usipitwe na breaking news mbalimbaliza michezo pamoja na tetesi zote za usajili,like page yetu ya facebook 👉👉 HAPA


Lipuli ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda daraja msimu uliopita na imeanza kujipanga kwa msimu wa Ligi Kuu kwa kumpa Matola mkataba wa mwaka mmoja

Sasa dili limekamilika baada ya aliyekuwa kocha msaidizi wa zamani wa Simba Selemani Matola, kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Lipuli ya Iringa ambayo itashiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Matola ameiambia Goal, hiyo ni kazi kubwa na ngumu lakini amejipanga kuhakikisha anaipa mafanikio timu hiyo katika kipindi atakachokuwa klabuni hapo.

“Ni kazi ngumu kwa sababu Lipuli ni timu ndogo na ngeni kwenye ligi na msimu ujao unatabiriwa kuwa mgumu lakini nitajitahidi kwa kushirikiana na viongozi wa timu kuhakikisha tunafanya vizuri,” amesema Matola.

Kocha huyo ambaye pia aliwahi kuifundisha Geita Gold Mine ya Geita amesema kazi yake kubwa hivi sasa itakuwa ni kukiimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Amesema katika kikosi chake anahitaji kuwa na wachezaji wazoeafu wasiopungua watano ambao atawachanganya na chipukizi wengine walioipandisha timu ili kujenga mchanganyiko mzuri.

“Najua ligi itakuwa ngumu lakini kama tutafanikiwa kusajili vizuri sioni kikwazo hapo naamini tutakuwa na kikosi imara na tutafanya vizuri kwa kutoa upinzani kama ilivyokuwa timu ngeni zilivyofanya vizuri huko nyuma.

Matola amesema hawezi kutoa ahadi kwa mashabiki na wakazi wa mkoa wa Iringa, lakini malengo yake ni kuhakikisha wanamaliza msimu bila kushuka daraja kabla ya kuwaza ubingwa msimu utakaofuata.


 Download app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉HAPA

No comments:

Post Bottom Ad

Pages