STARS KAMBINI TENA.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 12 June 2017

STARS KAMBINI TENA..


Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania 'Taifa Stars' itaingia kambini tena Juni 14, mwaka huu kujiandaa na michuano inayoratibiwa na Baraza la Soka la Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu ambako Taifa Stars itakwenda Afrika Kusini, Juni 20, mwaka huu.

Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amepanga kufanya mabadiliko madogo ya kikosi cha Taifa Stars kitakaochokwenda kushiriki michuano hiyo, kikosi ambacho kitawekwa hadharani kesho.

Timu hiyo imetoka kulazimishwa sare ya 1-1 na Lesotho katika mchezo wa kufuzu fainali za AFCON mwaka 2019, Jumamosi iliyopita.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages