Singano atoboa,akamilisha vipimo sasa kutimkia Morocco. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Wednesday, 28 June 2017

Singano atoboa,akamilisha vipimo sasa kutimkia Morocco.


Kiungo wa pembeni wa Azam FC, Ramadhani Singano amefuzu vipimo vya afya vya klabu ya Difaa Al Jadida ya Morocco.


Difaa Al Jadida ilimtumia mwakilishi wake nchini kumfanyia Singano maarufu kama Messi vipimo vya afya na taarifa zimeeleza kuwa amefuzu.
"Sasa ni suala la viza tu, kama hili likikamilika, basi Singano ataondoka. 

Hawataingia naye mkataba sasa hivi hadi mkataba wake na Azam FC utakapoisha siku chache zijazo.


"Ila kuna taarifa nimeambiwa wamemtaka kwenda kule mapema ili kuzoea mazingira," kilieleza chanzo.

Mkataba wa Singano na Azam FC umebakiza siku chache kwisha na hivi karibuni ilielezwa mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya Azam FCDown load app hii moja kwa moja kwenye kifaa chochote cha Android ili kupata habari kutoka vyankende.com 👉👉http://www.androidcreator.com/apk/app204631.apk

No comments:

Post Bottom Ad

Pages